Tarime: Heche azindua kampeni kwa kishindo, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on September 5, 2020 at 1:00 pm

September 5, 2020

Na Timoth Itembe-TarimeMGOMBEA ubunge Jimbo la Tarime Vijijini, John Heche (Chadema) ameiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Kutenda  haki kwa wagombea wote kadri wapiga kura watakavyokuwa wamewachagua viongozi wanaowapenda.Kauli hiyo aliitoa jana kwenye uzinduzi wa kampeni ndani ya Tarime vijijini kwenye viwanja vya Tarfa Sirari mpakani mwa nchi jirani ya Kenya mkutano ambao ulihudhuriwa na wagombea mbalimbali akiwemo Esther Matiko mgombea Ubunge jimbo la Tarime Mjini wagombea wengine, Julius Mwita (Musoma Mjini), Ester Bulaya (Bunda Mjini), Ezekiah Wenje (Rorya), Catherine Ruge (Serengeti) walihudhuria na kuwataka wananchi kutofanya kosa la kumchagua Waitara kwa kuwa ni msaliti na hana msiamamo.Heche alisema yeye ni muumini mkubwa  wa kutaka haki katika jambo lolote hivyo anatamani kuona uchaguzi wa mwaka huu ukifanyika kwa amani  na upendo hadi  matokeo yatakapotangazwa lakini anasikitishwa kuona baadhi ya viashiria kutoka kwa watumishi wa umma na jeshi la polisi wakifumbia macho bila kuwachukuliwa hatua baadhi ya kauli zinazotolewa na wapinzani wake.Alisema mpinzani wake ambaye ni Waitara  hana uwezo wala vigezo vya kumshinda katika sanduku la kura kutokana na tabia yake ya usaliti na utelekezaji wa  wananchi wa  jimbo la Ukonga jijini Dar s Salaam ambapo alimshauri kuanza kujifikiria kazi nyingine ya kufanya au kusubiria uteuzi wa nafasi 10 za upendelea kutoka kwa rais.“Ndani ya miaka mitano nimefanikiwa kujenga vituo vya afya tisa na hospitali moja inayomilikiwa na halmashauri, ipo pale Nyamwaga, kila shule ya sekondari na msingi nimepeleka saruji, mabati, mbao na misaada kadhaa ambayo yote ililenga kuondoa changamoto kwa wanafunzi wetu, wananchi wa Tarime Vijijini wote ni mashahidi kwa namna ninavyowapambania wananchi, sasa nashangaa mtu mmoja anakuja kusema yeye  anafaa wakati aliwatelekeza wananchi wa Ukonga.“Mimi nikishindwa na Waitara kwa haki nitakubali  kusaini na kwenda nyumbani kufanya shughuli zangu lakini kama kutakuwa na mtu anajaribu kuchezea kura zangu nipo tayari kuimbiwa wimbo wa parapanda italia, hili nalisema kwa uwazi kabisa maana nimeanza kusikia watendaji wanajigamba kwamba hawawezi kuwatangaza madiwani wa upinzani hata kama wameshinda.Mgombea huyo aliongeza kuwa yupo tayari kukubali matokeo ya kuzidiwa kura na mpinzani wake, Mwita Waitara (CCM) endapo haki na uwazi utatendeka huku akisisitiza kuwa ikitokea mtu kujaribu kuchezea kura zake yupo tayari kuimbiwa wimbo wa parapanda italia.Heche alisema endapo wananchi watamwamini na kumpa kura za kutosha atahakikisha barabara za lami zinajengwa katika baadhi ya  kata na kuwataka wananchi kumchangua mtu ambaye atakuwa mwakilishi wa wananchi siyo mwakilishi wa Serikali.Hata hivyo  wagombea  ubunge waliohudhuria  katika uzinduzi huo waliwataka wananchi  kumpa kura  mgombea urais  wa chama hicho, Tindu Lissu kama  pole ya kupigwa risasi 17 mwilini na kunusurika kifo.Walisema zawadi  pekee kwa Lissu amabye ni  mgombea urais  ni kumpa kura za kutosha  zitakazomwezesha kushinda nafasi hiyo na kuingia  Ikulu  na kuleta amani na uhuru kwa watanzania wote, vile vile waliwaomba kuwachagua madiwani wanaogombea kupitia Chadema ili kuweza kuongoza halmashauri.Wakati huo huo Mgombea Ubunge Jimbo la Serengeti Catherine Ruge alisema yeye anaushindi kwa sababu jina la Msubati linapendwa kutokana na elimu kutolewa na limetawala jimboni hapo ,,

Na Timoth Itembe-Tarime

MGOMBEA ubunge Jimbo la Tarime Vijijini, John Heche (Chadema) ameiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Kutenda  haki kwa wagombea wote kadri wapiga kura watakavyokuwa wamewachagua viongozi wanaowapenda.

Kauli hiyo aliitoa jana kwenye uzinduzi wa kampeni ndani ya Tarime vijijini kwenye viwanja vya Tarfa Sirari mpakani mwa nchi jirani ya Kenya mkutano ambao ulihudhuriwa na wagombea mbalimbali akiwemo Esther Matiko mgombea Ubunge jimbo la Tarime Mjini wagombea wengine, Julius Mwita (Musoma Mjini), Ester Bulaya (Bunda Mjini), Ezekiah Wenje (Rorya), Catherine Ruge (Serengeti) walihudhuria na kuwataka wananchi kutofanya kosa la kumchagua Waitara kwa kuwa ni msaliti na hana msiamamo.

Heche alisema yeye ni muumini mkubwa  wa kutaka haki katika jambo lolote hivyo anatamani kuona uchaguzi wa mwaka huu ukifanyika kwa amani  na upendo hadi  matokeo yatakapotangazwa lakini anasikitishwa kuona baadhi ya viashiria kutoka kwa watumishi wa umma na jeshi la polisi wakifumbia macho bila kuwachukuliwa hatua baadhi ya kauli zinazotolewa na wapinzani wake.

Alisema mpinzani wake ambaye ni Waitara  hana uwezo wala vigezo vya kumshinda katika sanduku la kura kutokana na tabia yake ya usaliti na utelekezaji wa  wananchi wa  jimbo la Ukonga jijini Dar s Salaam ambapo alimshauri kuanza kujifikiria kazi nyingine ya kufanya au kusubiria uteuzi wa nafasi 10 za upendelea kutoka kwa rais.

“Ndani ya miaka mitano nimefanikiwa kujenga vituo vya afya tisa na hospitali moja inayomilikiwa na halmashauri, ipo pale Nyamwaga, kila shule ya sekondari na msingi nimepeleka saruji, mabati, mbao na misaada kadhaa ambayo yote ililenga kuondoa changamoto kwa wanafunzi wetu, wananchi wa Tarime Vijijini wote ni mashahidi kwa namna ninavyowapambania wananchi, sasa nashangaa mtu mmoja anakuja kusema yeye  anafaa wakati aliwatelekeza wananchi wa Ukonga.

“Mimi nikishindwa na Waitara kwa haki nitakubali  kusaini na kwenda nyumbani kufanya shughuli zangu lakini kama kutakuwa na mtu anajaribu kuchezea kura zangu nipo tayari kuimbiwa wimbo wa parapanda italia, hili nalisema kwa uwazi kabisa maana nimeanza kusikia watendaji wanajigamba kwamba hawawezi kuwatangaza madiwani wa upinzani hata kama wameshinda.

Mgombea huyo aliongeza kuwa yupo tayari kukubali matokeo ya kuzidiwa kura na mpinzani wake, Mwita Waitara (CCM) endapo haki na uwazi utatendeka huku akisisitiza kuwa ikitokea mtu kujaribu kuchezea kura zake yupo tayari kuimbiwa wimbo wa parapanda italia.

Heche alisema endapo wananchi watamwamini na kumpa kura za kutosha atahakikisha barabara za lami zinajengwa katika baadhi ya  kata na kuwataka wananchi kumchangua mtu ambaye atakuwa mwakilishi wa wananchi siyo mwakilishi wa Serikali.

Hata hivyo  wagombea  ubunge waliohudhuria  katika uzinduzi huo waliwataka wananchi  kumpa kura  mgombea urais  wa chama hicho, Tindu Lissu kama  pole ya kupigwa risasi 17 mwilini na kunusurika kifo.

Walisema zawadi  pekee kwa Lissu amabye ni  mgombea urais  ni kumpa kura za kutosha  zitakazomwezesha kushinda nafasi hiyo na kuingia  Ikulu  na kuleta amani na uhuru kwa watanzania wote, vile vile waliwaomba kuwachagua madiwani wanaogombea kupitia Chadema ili kuweza kuongoza halmashauri.

Wakati huo huo Mgombea Ubunge Jimbo la Serengeti Catherine Ruge alisema yeye anaushindi kwa sababu jina la Msubati linapendwa kutokana na elimu kutolewa na limetawala jimboni hapo ,

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *