TARI yawakumbusha wakulima wa korosho umuhimu wa kuimarisha ubora, on September 20, 2020 at 1:00 pm

September 20, 2020

 Na Ahmad Mmow, Lindi.Wakulima wa korosho nchini wamehimizwa na kukumbushwa waimarishe ubora wa korosho ili zao hilo liweze kuwa na soko zuri litakalosababisha wawe na tija kutokana na kazi wanazofanya.Wito huo ulitolewa juzi na mkurugenzi wa utafiti wa mazao ya kilimo nchini(TARI), Dkt Fortunatus Kapinga wakati wa mkutano wa wadau wa korosho, ufuta na mbaazi kwa mkoa wa Lindi. Mkutano ambao uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Lindi uliopo katika manispaa ya Lindi.Dkt Kapinga alisema ili zao hilo liweze kuwa na soko zuri litakalosababisha bei kuwa nzuri ni ubora utakaosababisha wanunuzi washindanie kununua. Kwahiyo wakulima hawanabudi kuimarisha ubora katika hatua zote hadi kufikia hatua ya kuuza.Mkurugenzi huyo aliwaasa wakulima ambao korosho zao wanazianika kwakumwaga chini waache tabia hiyo. Bali waanike kwenye maturubai na sakafuni. Kwani kuanika kwenye mchanga na udongo kunasababisha korosho kuchanganyika na mchanga, udongo, kokoto na takataka nyingine ambazo hazihitajiki.Dkt Kapinga pia aliwaasa wakulima watunze korosho kwenye magunia badala ya viloba. Kwani viloba sio vifungashio sahihi na havifai kuhifadhia zao hilo. Kwani vinahifdhi unyevu.” Hatuwezi kufika kwenye viwango vinavyohitajika ikiwa korosho zetu zina takataka na uchafu ambao unapunguza kiwango cha ubora unaohitajika,” alisisitiza na kuonya Dkt Kapinga.Dkt Kapinga ambae alishangazwa na changamoto ya kuchelewa kusambazwa magunia kwa vyama vya msingi vya ushirika(AMCOS) na wakulima alitoa wito wakuwepo muda maalumu na wa mwisho wakuletwa magunia ili kuepukanana changamoto ya kuchelewa kusambazwa kwa wakulima ambao kutokana na kushindwa kupata magunia wanatumia viloba kuhifadhia korosho zao.Aidha Mkurugenzi huyo wa taasisi ya utafiti wa mazao ya kilimo nchini kituo cha Naliendele kilichopo mkoani Mtwara alisema TARI inaamini Mkoa wa Lindi unauwezo mkubwa wa kuzalisha kwa wingi zao hilo. Nikutokanana mkoa huo kuwa na maeneo bora na makubwa yanayofaa kwa kilimo cha korosho.Mbali na hayo mtaalamu huyo wa kilimo alishukukuru serikali ya mkoa wa Lindi kwa ushirikiano mkubwa na taasisi hiyo. Hivyo aliahidi taasisi hiyo kuendelea kutoa ushirikiano na serikali ya mkoa huo. Huku akitoa wito iwahamasishe  wakulima waanze kulima alizeti.,

 

Na Ahmad Mmow, Lindi.

Wakulima wa korosho nchini wamehimizwa na kukumbushwa waimarishe ubora wa korosho ili zao hilo liweze kuwa na soko zuri litakalosababisha wawe na tija kutokana na kazi wanazofanya.

Wito huo ulitolewa juzi na mkurugenzi wa utafiti wa mazao ya kilimo nchini(TARI), Dkt Fortunatus Kapinga wakati wa mkutano wa wadau wa korosho, ufuta na mbaazi kwa mkoa wa Lindi. Mkutano ambao uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Lindi uliopo katika manispaa ya Lindi.

Dkt Kapinga alisema ili zao hilo liweze kuwa na soko zuri litakalosababisha bei kuwa nzuri ni ubora utakaosababisha wanunuzi washindanie kununua. Kwahiyo wakulima hawanabudi kuimarisha ubora katika hatua zote hadi kufikia hatua ya kuuza.

Mkurugenzi huyo aliwaasa wakulima ambao korosho zao wanazianika kwakumwaga chini waache tabia hiyo. Bali waanike kwenye maturubai na sakafuni. Kwani kuanika kwenye mchanga na udongo kunasababisha korosho kuchanganyika na mchanga, udongo, kokoto na takataka nyingine ambazo hazihitajiki.

Dkt Kapinga pia aliwaasa wakulima watunze korosho kwenye magunia badala ya viloba. Kwani viloba sio vifungashio sahihi na havifai kuhifadhia zao hilo. Kwani vinahifdhi unyevu.

” Hatuwezi kufika kwenye viwango vinavyohitajika ikiwa korosho zetu zina takataka na uchafu ambao unapunguza kiwango cha ubora unaohitajika,” alisisitiza na kuonya Dkt Kapinga.

Dkt Kapinga ambae alishangazwa na changamoto ya kuchelewa kusambazwa magunia kwa vyama vya msingi vya ushirika(AMCOS) na wakulima alitoa wito wakuwepo muda maalumu na wa mwisho wakuletwa magunia ili kuepukanana changamoto ya kuchelewa kusambazwa kwa wakulima ambao kutokana na kushindwa kupata magunia wanatumia viloba kuhifadhia korosho zao.

Aidha Mkurugenzi huyo wa taasisi ya utafiti wa mazao ya kilimo nchini kituo cha Naliendele kilichopo mkoani Mtwara alisema TARI inaamini Mkoa wa Lindi unauwezo mkubwa wa kuzalisha kwa wingi zao hilo. Nikutokanana mkoa huo kuwa na maeneo bora na makubwa yanayofaa kwa kilimo cha korosho.

Mbali na hayo mtaalamu huyo wa kilimo alishukukuru serikali ya mkoa wa Lindi kwa ushirikiano mkubwa na taasisi hiyo. Hivyo aliahidi taasisi hiyo kuendelea kutoa ushirikiano na serikali ya mkoa huo. Huku akitoa wito iwahamasishe  wakulima waanze kulima alizeti.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *