Tanzania Yatajwa Nchi ya Kwanza kwa Amani Afrika Mashariki, noreply@blogger.com (Udaku Special)

August 31, 2020

JAMHURI ya Muungano wa Tanzania imetajwa kuwa ndiyo nchi ya kwanza (inayoongoza) kwa kuwa na amani katika Ukanda wa Afrika Mashariki.Kwa mujibu wa jarida la Kimataifa la Global Peace Index limetoa takwimu za mwaka 2020 zikionyesha kuwa Tanzania imepanda juu huku ikiwa ya sita kwa Afrika na ikishika nafasi ya 52 duniani kote.Kwa mujibu wa jarida hilo,  eneo la kusini mwa Jangwa la Sahara limepungua kwa kiasi kidogo mazingira ya amani na usalama kwa asilimia  0.5.Nchi 20 katika eneo hilo zimeimarika kiwango chake cha amani na lakini nchi 24 zimepungua kiwango chake cha mazingira ya amani.Migogoro kuhusu matokeo ya uchaguzi na madai ya kuwepo mabadiliko ya kisiasa, yamesababisha machafuko na vurugu za kisiasa katika nchi kadhaa eneo hilo ikiwa ni pamoja na maandamano ya vurugu mnamo mwaka uliopita.,

JAMHURI ya Muungano wa Tanzania imetajwa kuwa ndiyo nchi ya kwanza (inayoongoza) kwa kuwa na amani katika Ukanda wa Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa jarida la Kimataifa la Global Peace Index limetoa takwimu za mwaka 2020 zikionyesha kuwa Tanzania imepanda juu huku ikiwa ya sita kwa Afrika na ikishika nafasi ya 52 duniani kote.

Kwa mujibu wa jarida hilo,  eneo la kusini mwa Jangwa la Sahara limepungua kwa kiasi kidogo mazingira ya amani na usalama kwa asilimia  0.5.

Nchi 20 katika eneo hilo zimeimarika kiwango chake cha amani na lakini nchi 24 zimepungua kiwango chake cha mazingira ya amani.

Migogoro kuhusu matokeo ya uchaguzi na madai ya kuwepo mabadiliko ya kisiasa, yamesababisha machafuko na vurugu za kisiasa katika nchi kadhaa eneo hilo ikiwa ni pamoja na maandamano ya vurugu mnamo mwaka uliopita.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *