Tanzania yapokea kichapo kutoka kwa Burundi,

October 11, 2020

 

Timu ya taifa ya soka ya Tanzania, imekubali kichapo cha goli 1-0 kutoka kwa Burundi kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam.

Tanzania ilikosa nafasi kadhaa kipindi cha kwanza na cha pili kupitia kwa nyota wake Simon Msuva, Mbwana Samatta na wengine kabla ya Burundi kutumia nafasi.

Dakika ya 80 kiungo wa Tanzania na klabu ya Simba Jonas Mkude alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kuwa na majizano na mshambuliaji Saido Berahino.

Dakika ya 86 mshambuliaji wa Burundi Saidi Ntibazonkiza akaifungia goli timu yake ambalo limedumu mpaka dakika 90 zinamalizika.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *