Tanasha Gumzo Kuolewa Mke wa Pili, noreply@blogger.com (Udaku Special)

September 5, 2020

MAMBO ni moto huko nchini Kenya, baada ya mzazi mwenza wa msanii maarufu wa Bongo Fleva nchini, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Tanasha Donna kudaiwa kutaka kufunga ndoa na mtangazaji maarufu wa televisheni nchini humo, Jamal Gaddafi.Gaddafi ambaye tayari ana mke na watoto wawili, alianza kuonekana hadharani na Tanasha kuanzia Mei mwaka huu wakati wa mfungo wa Ramadhani, ambapo Tanasha alikuwa akishiriki futari, pamoja na familia ya mtangazaji huyo.Hata hivyo, sasa hivi wawili hao wameelezwa kupika na kupakua pamoja, jambo ambalo limezidi kupigia mstari uwepo wa ndoa ya pili kwa Jamal, hasa ikizingatiwa dini ya Kiislamu inamruhusu.Pamoja na hayo, wafuasi wao hususani kwenye mitandao ya kijamii, wameunga mkono ‘couple’ hiyo na kumtaka Gaddafi kumuoa Tanasha.Aidha, Gaddafi alipoulizwa kituo kimoja na televisheni kuhusu uwezekano wa kuoa mke wa pili, alikiri kuwa nafasi hiyo ipo kwa sababu mke wake amempa baraka zote za kuongeza mke, jambo ambalo linaonekana kuchagiza uwezekano wa kumuoa Tanasha.Wakati ukaribu wao ukizua gumzo, hivi karibuni Jamal amepakia kwenye akaunti yake ya Instagram, video akiwa amembeba mtoto wa Diamond, Naseeb Junior, huku Tanasha akiwa nyuma yao, jambo ambalo linadhihirisha ukaribu wao.Licha ya mengi kusemwa kuhusu uhusiano wao, Tanasha alipohojiwa na kituo cha Jambo Radio nchini humo, mbali na kudai uhusiano wao ni wa kaka na dada, alisema Jamal ni miongoni mwa watu ambao wamemsaidia kukamilisha na kuendeleza miradi yake.Hata hivyo, ukaribu umezidi kuimarika kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele, baada ya familia ya Jamal kumkubali na kumkaribisha Tanasha kama sehemu ya familia yao, jambo lililowanyamazisha wakosoaji wengi.Vyanzo mbalimbali vimeeleza kuwa, wawili hao wamekuwa wakitumia muda mrefu kujirusha pamoja na kutumia nafasi zao kutekeleza majukumu yao kama timu moja.Kama hiyo haitoshi, katika akaunti ya mtoto huyo wa Mondi, Naseeb Junior imemtambulisha Jamal kama Mjomba wake kwa mujibu wa picha ambazo zimepostiwa kwenye akaunti hiyo.JAMAL AWEKWA MTU KATIWakati Jamal akiendelea kuposti picha zake na Tanasha mitandaoni hususani Instagram na kusindikiza na maneno ya kumchombeza, baadhi ya wananchi wamemuuliza kama kweli anampenda Tanasha au lah!Jamal aliposti picha ya Tanasha na kuandika, “Hauwezi kufanya watu wote wakupende, wakukubali au waamini wema wako… kwa sababu hauna uwezo wa kuControl mawazo yao.Lakini habari njema katika hili ni kwamba, “It doesn’t matter kabisa” wewe kula vizuri, kunywa maji ya kutosha bila kusahau machungwa, enjoy maisha.”Aidha, wafuasi wake kwenye mtandao huo akiwamo, Marimar Dixon alimuuliza unampenda Tanasha, na Jamal akajibu ndiyo. Marimardixon alihoji, “Hey Jamal! do u love Tanasha? Na Jamal akajibu, ‘Nampenda sana’.AMBADILISHA TANASHAAidha, uhusiano wao umeelezwa kuzidi kumjenga Tanasha, kimuziki na kimaadili, ambapo mbali na Jamal kumsaidia mrembo huyo katika kazi zake, pia muonekano wake umezidi kuwa tofauti.Wachambuzi wa masuala ya burudani, wanaeleza kuwa awali Tanasha alikuwa mtoto wa mjini kwamba, alikuwa akivaa mavazi yasiyostiri mwili, sasa imekuwa ni tofauti ambapo anavaa mavazi yenye heshima kuzingatia maadili ya dini ya Kiislamu.Jamal pia anatajwa kumbadilisha Tanasha kwa kuwa mtu wa kijamii zaidi kwa kushiriki matukio kama vile ya kutembelea vituo vya watoto yatima na kumsaidia kuanzisha taasisi yake ya Tanasha Donna Community Service,

MAMBO ni moto huko nchini Kenya, baada ya mzazi mwenza wa msanii maarufu wa Bongo Fleva nchini, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Tanasha Donna kudaiwa kutaka kufunga ndoa na mtangazaji maarufu wa televisheni nchini humo, Jamal Gaddafi.

Gaddafi ambaye tayari ana mke na watoto wawili, alianza kuonekana hadharani na Tanasha kuanzia Mei mwaka huu wakati wa mfungo wa Ramadhani, ambapo Tanasha alikuwa akishiriki futari, pamoja na familia ya mtangazaji huyo.

Hata hivyo, sasa hivi wawili hao wameelezwa kupika na kupakua pamoja, jambo ambalo limezidi kupigia mstari uwepo wa ndoa ya pili kwa Jamal, hasa ikizingatiwa dini ya Kiislamu inamruhusu.

Pamoja na hayo, wafuasi wao hususani kwenye mitandao ya kijamii, wameunga mkono ‘couple’ hiyo na kumtaka Gaddafi kumuoa Tanasha.

Aidha, Gaddafi alipoulizwa kituo kimoja na televisheni kuhusu uwezekano wa kuoa mke wa pili, alikiri kuwa nafasi hiyo ipo kwa sababu mke wake amempa baraka zote za kuongeza mke, jambo ambalo linaonekana kuchagiza uwezekano wa kumuoa Tanasha.

Wakati ukaribu wao ukizua gumzo, hivi karibuni Jamal amepakia kwenye akaunti yake ya Instagram, video akiwa amembeba mtoto wa Diamond, Naseeb Junior, huku Tanasha akiwa nyuma yao, jambo ambalo linadhihirisha ukaribu wao.

Licha ya mengi kusemwa kuhusu uhusiano wao, Tanasha alipohojiwa na kituo cha Jambo Radio nchini humo, mbali na kudai uhusiano wao ni wa kaka na dada, alisema Jamal ni miongoni mwa watu ambao wamemsaidia kukamilisha na kuendeleza miradi yake.

Hata hivyo, ukaribu umezidi kuimarika kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele, baada ya familia ya Jamal kumkubali na kumkaribisha Tanasha kama sehemu ya familia yao, jambo lililowanyamazisha wakosoaji wengi.

Vyanzo mbalimbali vimeeleza kuwa, wawili hao wamekuwa wakitumia muda mrefu kujirusha pamoja na kutumia nafasi zao kutekeleza majukumu yao kama timu moja.

Kama hiyo haitoshi, katika akaunti ya mtoto huyo wa Mondi, Naseeb Junior imemtambulisha Jamal kama Mjomba wake kwa mujibu wa picha ambazo zimepostiwa kwenye akaunti hiyo.

JAMAL AWEKWA MTU KATI

Wakati Jamal akiendelea kuposti picha zake na Tanasha mitandaoni hususani Instagram na kusindikiza na maneno ya kumchombeza, baadhi ya wananchi wamemuuliza kama kweli anampenda Tanasha au lah!

Jamal aliposti picha ya Tanasha na kuandika, “Hauwezi kufanya watu wote wakupende, wakukubali au waamini wema wako… kwa sababu hauna uwezo wa kuControl mawazo yao.

Lakini habari njema katika hili ni kwamba, “It doesn’t matter kabisa” wewe kula vizuri, kunywa maji ya kutosha bila kusahau machungwa, enjoy maisha.”

Aidha, wafuasi wake kwenye mtandao huo akiwamo, Marimar Dixon alimuuliza unampenda Tanasha, na Jamal akajibu ndiyo. Marimardixon alihoji, “Hey Jamal! do u love Tanasha? Na Jamal akajibu, ‘Nampenda sana’.

AMBADILISHA TANASHA

Aidha, uhusiano wao umeelezwa kuzidi kumjenga Tanasha, kimuziki na kimaadili, ambapo mbali na Jamal kumsaidia mrembo huyo katika kazi zake, pia muonekano wake umezidi kuwa tofauti.

Wachambuzi wa masuala ya burudani, wanaeleza kuwa awali Tanasha alikuwa mtoto wa mjini kwamba, alikuwa akivaa mavazi yasiyostiri mwili, sasa imekuwa ni tofauti ambapo anavaa mavazi yenye heshima kuzingatia maadili ya dini ya Kiislamu.

Jamal pia anatajwa kumbadilisha Tanasha kwa kuwa mtu wa kijamii zaidi kwa kushiriki matukio kama vile ya kutembelea vituo vya watoto yatima na kumsaidia kuanzisha taasisi yake ya Tanasha Donna Community Service

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *