Takwimu zinaiumiza Kagera Sugar dhidi ya Yanga

September 19, 2020

Klabu ya Kagera Sugar itakua mwenyeji wa Yanga hii leo katika muendelezo wa michuano ya Ligi kuu ya Tanzania Bara ambayo imeingia katika raundi yake ya tatu.Kagera inayonolewa na Kocha Mecky mexime,inausaka ushindi wake wa kwanza msimu huu kufuatia kupoteza mechi yake ya kwanza nyumbani dhidi ya JKT Tanzania kwa bao 1-0 na kutoka suluhu ugenini dhidi ya Gwambina.Yanga wao watakua wakihitaji ushindi wa pili mfululizo baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya Mbeya City na sare ya bao 1-1 na Tanzania Prisons.Msimu uliopita, Kagera iliiadabisha Yanga katika Uwanja wa Mkapa kwa kuwalaza bao 3-0 lakini Yanga walijibu kiasi kwa kushinda Kaitaba kwa bao 1-0.Kuelekea mchezo wa leo utakaopigwa katika Uwanja wa Kaitaba,East Africa Radio inakusogezea takwimu za mechi tano za mwisho baina ya miamba hiyo miwili ya soka ilipokutana katika Uwanja wa Kaitaba.2015/16-Kagera 0-2 Yanga2016/17- Kagera 0-2 Yanga2017/18-Kagera 2-6 Yanga2018/19-Kagera1-2 Yanga2019/20-Kagera 0-1 YangaYanga Sc haijapoteza mchezo wowote katika mechi tano za mwisho dhidi ya Kagera Sugar katika uwanja wa Kaitaba,

Klabu ya Kagera Sugar itakua mwenyeji wa Yanga hii leo katika muendelezo wa michuano ya Ligi kuu ya Tanzania Bara ambayo imeingia katika raundi yake ya tatu.

Kagera inayonolewa na Kocha Mecky mexime,inausaka ushindi wake wa kwanza msimu huu kufuatia kupoteza mechi yake ya kwanza nyumbani dhidi ya JKT Tanzania kwa bao 1-0 na kutoka suluhu ugenini dhidi ya Gwambina.

Yanga wao watakua wakihitaji ushindi wa pili mfululizo baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya Mbeya City na sare ya bao 1-1 na Tanzania Prisons.

Msimu uliopita, Kagera iliiadabisha Yanga katika Uwanja wa Mkapa kwa kuwalaza bao 3-0 lakini Yanga walijibu kiasi kwa kushinda Kaitaba kwa bao 1-0.

Kuelekea mchezo wa leo utakaopigwa katika Uwanja wa Kaitaba,East Africa Radio inakusogezea takwimu za mechi tano za mwisho baina ya miamba hiyo miwili ya soka ilipokutana katika Uwanja wa Kaitaba.

2015/16-Kagera 0-2 Yanga

2016/17- Kagera 0-2 Yanga

2017/18-Kagera 2-6 Yanga

2018/19-Kagera1-2 Yanga

2019/20-Kagera 0-1 Yanga

Yanga Sc haijapoteza mchezo wowote katika mechi tano za mwisho dhidi ya Kagera Sugar katika uwanja wa Kaitaba

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *