Takukuru Mkoa wa Mtwara yarejesha milioni 56,416,00 za baadhi ya wafanyakazi wa kampuni za ulinzi za Kiwango pamoja na Consultancy.,

October 13, 2020

 

Na Faruku Ngonyani ,Mtwara

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)Mkoa wa Mtwara imefanikiwa kuwarejeshea kiasi cha Shilingi Milioni Hamsini na Sita Laki Nne kumi na sita elfu(56,410,600) za michango kutoka kwa watumishi Mbali mbali wa kampuni za ulinzi za Kiwango Security Gurd na Unique Consultancy Company Ltd Mtwara ambazo zote zinawajika katika kiwanda cha Saruji cha Dangote Mkoani Mtwara.

Akuzungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa Takukuru Mkoa wa Mtwara Enock Ngailo amesema kuwa ofisi yake ilipata malalamiko kutoka kwa baadhi ya  watumishi mbali mbali wa kampuni hizo wakilalamikia juu ya kukatwa fedha hizo za michango kwenye mfuko wa hifadhi ya Jamii (NSSF).

Hatimae Takukuru waliitisha vikao vya pamoja kati ya waajiri ,NSSF  na hatamae kufanikiwa kukubaliana fedha hizo zitolewe na kukabidhiwa kwa waajiriwa hao.

‘Baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hizi mbili Takukuru Mkoa wa Mtwara tulifanya kikao cha pamoja na NSSF pamoja waajiri na hatimae tukakubaliana kiasi cha sh. 56,426,000 kilichokatwa kiweze kureshwa kwa wahusika’

Aidha TAKUKURU Mkoa wa Mtwara kwa kipindi cha miezi Mitatu(3) kuanzia Juai 2020 hadi Septemba  imefanikiwa kukusanya jumla ya taarifa 145 za makossa mbali mbali ya Rushwa na Jinai ,ambapo uchunguzi wake bado unaendelea  huko mahakani dhidi ya watuhumiwa wa makossa hayo .

Lakini pia Kamanda Ngailo amezichanganua kesi hizo ambapo kwa Halmashauri kuna jumla ya malalmiko (43) katika idara zake za Utawala  malalamiko (11) Ardhi (7), Elimu (7), Biashara (6) ,Maji (4) Kilimo (3) ,Afya (2) Ujenzi (2) , na Umishi lalamiko (1)

Malalamiko mengine kupitia vyama vya Ushirika ambapo yapo (29) , Siasa (26) , Mifuko ya hifadhi ya Jamii (15) , Mahakama (6) Mawasiliano (6), Polisi (2) ,Dini (2), TPA (1), Michezo (1), uhamiaji (1) na binafsi (1).

‘Nitoe wito kwa watumishi wote wa Halmashuri zote zilizopo Mkoani Mtwara na Viongozi wa Ushirika kufanya kazoo kwa uadilifu na kwa kuzingatia sharia,kanuni na tyaratibu kwani takwimu za taarifa za malalmiko dhidi yao ni kubwa, KATAA RUSHWA ,JENGA TANZANIA’

Aidha TAKUKURU Mkoa wa Mtwara kwa kipindi cha miezi mitatu wamefanikwa kurejesha Zaidi milioni sabuni na mbili zilizotokana na mapunjo ya zao la korosho katika Misimu mbali mbali Mkaoni Mtwara.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *