Syria: Marekani yapeleka vikosi zaidi baada ya kuzozana na Urusi, on September 19, 2020 at 3:00 pm

September 19, 2020

 Marekani imeongeza idadi ya wanajeshi wake Syria baada ya malumbano kati yake na Urusi kuzua hali ya taharuki nchini humo.Maafisa wa Marekani wanesema magari sita ya vita na karibu wanajeshi 100 wamepelekwa kaskazini mashariki mwa Syria.Visa vya makabiliano kati ya vikosi vya Marekani na Urusi vinavyoweka ulinzi katika nchi hiyo vimeongezeka mwaka huu.Kapteni wa jeshi la majni la Marekani Bill Urban amesema hatua hiyo itasaidia “kuhakikisha usalama wa vikosi vya muungano”.Ameongeza kuwa, pamoja na magari hayo ya vita amabyo yalikuwa Kuwait, Marekani pia itapeleka “Vifaa vya ulizi wa angani” na kuongeza “doria za mara kwa mara ya doria zinazofanywa dhidi ya vikosi hivyo”.”Marekani haina mpago wa kuzozana na nchi nyingine Syria, lakini italinda vikosi vya muungano ikilazimika kufanya hivyo,” Bwana Urban, ambaye ni msemaji wa majeshi ya Marekani alisema, katika taarifa siku ya Ijumaa.Bwana Urban hakutaja Urusi kwa jina, lakini katika taarifa nyingine kutoka kwa maafisa wa Marekani, iliyoangaziwa kwanza na kituo cha habari cha NBC, aliashiria anazungumzia nchi hiyo.”Hatua hii inatuma “ishara kwa Urusi” kujiepusha na vitendo vya “uchokozi” kaskazini mashariki mwa Syria,” alisema afisa mmoja ambaye jina lake halikutajwa.Kituo cha NBC kiliwanukuu maafisa hao wakidaiwa kusema kwamba wanajeshi zaidi na magari ya kivita yamepelekwa kaskazini mashariki mwa Syria ili kuzuia vikosi vya Urusi kuingia katika maeneo ya usalama ambako vikosi vya Muungano vya Marekani vikosi vya Kikurdi vinaendesha oparesheni.Kwa miaka kadhaa sasa, kumeshuhudiwa mzozo wa mara kwa mara kati ya vikozi vya Marekani na Urusi nchini Syria. Lakini matukio ya wiki za hivi karibuni kaskazini mashariki mwa Syria vimeongeza uhasama kati ya nchi hizo mbili.Mwisho wa mwezi Agosti, wanajeshi saba wa Marekani walijeruhiwa baada ya gari lao kugonhgana na gari la kijeshi la Urusi. Serikali za Urusi na Marekani zililaumiana kufuatia tukio hilo ambalo lilinaswa kwenye kanda ya video na kuwekwa katika mtandao wa kijamii wa Twitter.Video hiyo inaonesha gari la kijeshi la Urusi katika msafara wa jangwani ukigongana na gari la kijeshi la Marekani, Helikopta ya Urusi ilipaa umbali wa chini kabisa.Urusi inasema kuwa Marekani ilizuia doria.,

 

Marekani imeongeza idadi ya wanajeshi wake Syria baada ya malumbano kati yake na Urusi kuzua hali ya taharuki nchini humo.

Maafisa wa Marekani wanesema magari sita ya vita na karibu wanajeshi 100 wamepelekwa kaskazini mashariki mwa Syria.

Visa vya makabiliano kati ya vikosi vya Marekani na Urusi vinavyoweka ulinzi katika nchi hiyo vimeongezeka mwaka huu.

Kapteni wa jeshi la majni la Marekani Bill Urban amesema hatua hiyo itasaidia “kuhakikisha usalama wa vikosi vya muungano”.

Ameongeza kuwa, pamoja na magari hayo ya vita amabyo yalikuwa Kuwait, Marekani pia itapeleka “Vifaa vya ulizi wa angani” na kuongeza “doria za mara kwa mara ya doria zinazofanywa dhidi ya vikosi hivyo”.

“Marekani haina mpago wa kuzozana na nchi nyingine Syria, lakini italinda vikosi vya muungano ikilazimika kufanya hivyo,” Bwana Urban, ambaye ni msemaji wa majeshi ya Marekani alisema, katika taarifa siku ya Ijumaa.

Bwana Urban hakutaja Urusi kwa jina, lakini katika taarifa nyingine kutoka kwa maafisa wa Marekani, iliyoangaziwa kwanza na kituo cha habari cha NBC, aliashiria anazungumzia nchi hiyo.

“Hatua hii inatuma “ishara kwa Urusi” kujiepusha na vitendo vya “uchokozi” kaskazini mashariki mwa Syria,” alisema afisa mmoja ambaye jina lake halikutajwa.

Kituo cha NBC kiliwanukuu maafisa hao wakidaiwa kusema kwamba wanajeshi zaidi na magari ya kivita yamepelekwa kaskazini mashariki mwa Syria ili kuzuia vikosi vya Urusi kuingia katika maeneo ya usalama ambako vikosi vya Muungano vya Marekani vikosi vya Kikurdi vinaendesha oparesheni.

Kwa miaka kadhaa sasa, kumeshuhudiwa mzozo wa mara kwa mara kati ya vikozi vya Marekani na Urusi nchini Syria. Lakini matukio ya wiki za hivi karibuni kaskazini mashariki mwa Syria vimeongeza uhasama kati ya nchi hizo mbili.

Mwisho wa mwezi Agosti, wanajeshi saba wa Marekani walijeruhiwa baada ya gari lao kugonhgana na gari la kijeshi la Urusi. Serikali za Urusi na Marekani zililaumiana kufuatia tukio hilo ambalo lilinaswa kwenye kanda ya video na kuwekwa katika mtandao wa kijamii wa Twitter.

Video hiyo inaonesha gari la kijeshi la Urusi katika msafara wa jangwani ukigongana na gari la kijeshi la Marekani, Helikopta ya Urusi ilipaa umbali wa chini kabisa.

Urusi inasema kuwa Marekani ilizuia doria.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *