Sudan yakubali kurudisha uhusiano wake na Israel,

October 16, 2020

Serikali ya Sudan inadaiwa kukubali pendekezo la Marekani linalohimiza utawala wa Khartoum kurudisha uhusiano na Israel, ili waweze kutia saini mkataba wa makubaliano.

Kwa mujibu wa taarifa za kituo cha televisheni cha 124News, ilidaiwa kuwa viongozi wa Marekani na Sudan walikutana hapo jana kujadili suala la kurudisha uhusiano mzuri kati ya utawala wa Khartoum na Israel.

Taarifa zaidi zinaarifu kwamba upande wa Marekani ulitoa muda wa masaa 24 kwa Sudan ili watoe majibu kuhusu pendekezo la kurudisha uhusiano mzuri kati ya utawala wa Khartoum na Israel.

Wakati huo huo, ilibainishwa kuwa Marekani pia iliahidi kuindoa Sudan kwenye orodha ya nchi zinazounga mkono ugaidi endapo itarudisha uhusiano wake na Israel.

Licha ya Sudan kudaiwa kukubaliana na pendekezo hilo, mamlaka husika bado haijatoa maelezo yoyote kuhusu suala hilo.

Mnamo mwezi uliopita, viongozi wa Sudan na Marekani walifanya mkutano Abu Dhabi na kujadili suala la utawala wa Khartoum kurudisha uhusiano na Israel ingawa mazungumzo hayo hayakuzaa matunda.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *