Sudan yafikia mkataba wa amani na waasi, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on August 31, 2020 at 1:00 pm

August 31, 2020

Hafla ya kutia saini mkataba wa amani ilifanyika Sudan KusiniImage caption: Hafla ya kutia saini mkataba wa amani ilifanyika Sudan KusiniSerikali ya mpito ya Sudan imetia saini mkataba wa amani na makundi ya waasi katika hafla iliyoandaliwa nchi jirani ya Sudan Kusini.Mkataba huo unalenga kumaliza mzozo wa mika 17 katika maeneo ya magharibi mwa Darfur na majimbo ya kusini.Hii ni hatua kubwa kuelekea kutafuta ufumbuzi wa mizozo kadhaa nchi humo,anasema mwandishi wa BBC Anne Soy.Hata hivyo makundi mawili muhimu ya waasi yamekataa kutia saini mkataba huo ambao unaangazia masuala ya kama vile umiliki wa ardhi, ugawanaji mamlaka na jinsi mamilioni ya watu waliotoroka makwao kutokana na mapigano watakavyorejea nyumbani.Makundi ya waasi mjini Darfur yalianza kupigana na vikosi vya serikali 2003Image caption: Makundi ya waasi mjini Darfur yalianza kupigana na vikosi vya serikali 2003Makubaliano yaliopita ya amani yaliolenga kukomesha mzozo huo wa muda mrefu yalitibuka.Mapigano kati ya vikosi vya serikali na waasi yalianza 2003 na yamesababisha vifo vya maelfu ya watu huku mamilioni ya wengine yakifurushwa makwao.Mazungumzo ya Amani yalicheleweshwa mara kadhaa kufuatia kifo cha waziri wa ulinzi wa zamani wa Sudan, Jamaleldin Omar, na janga la Covid-19.,

Hafla ya kutia saini mkataba wa amani ilifanyika Sudan KusiniImage caption: Hafla ya kutia saini mkataba wa amani ilifanyika Sudan Kusini

Serikali ya mpito ya Sudan imetia saini mkataba wa amani na makundi ya waasi katika hafla iliyoandaliwa nchi jirani ya Sudan Kusini.

Mkataba huo unalenga kumaliza mzozo wa mika 17 katika maeneo ya magharibi mwa Darfur na majimbo ya kusini.

Hii ni hatua kubwa kuelekea kutafuta ufumbuzi wa mizozo kadhaa nchi humo,anasema mwandishi wa BBC Anne Soy.

Hata hivyo makundi mawili muhimu ya waasi yamekataa kutia saini mkataba huo ambao unaangazia masuala ya kama vile umiliki wa ardhi, ugawanaji mamlaka na jinsi mamilioni ya watu waliotoroka makwao kutokana na mapigano watakavyorejea nyumbani.

Makundi ya waasi mjini Darfur yalianza kupigana na vikosi vya serikali 2003Image caption: Makundi ya waasi mjini Darfur yalianza kupigana na vikosi vya serikali 2003

Makubaliano yaliopita ya amani yaliolenga kukomesha mzozo huo wa muda mrefu yalitibuka.

Mapigano kati ya vikosi vya serikali na waasi yalianza 2003 na yamesababisha vifo vya maelfu ya watu huku mamilioni ya wengine yakifurushwa makwao.

Mazungumzo ya Amani yalicheleweshwa mara kadhaa kufuatia kifo cha waziri wa ulinzi wa zamani wa Sudan, Jamaleldin Omar, na janga la Covid-19.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *