Staa WNBA Aolewa na Mwanamme Aliyemtoa Gerezani

September 17, 2020

MCHEZAJI nyota wa mpira wa kikapu nchini Marekani, Maya Moore, ameolewa na Jonathan Irons mwanamme aliyemsaidia kumuondoa jela baada ya kufungwa bila hatia.Irons aliachiliwa huru tarehe 23 Julai baada ya kufungwa  miaka 23, na baadaye kubainika kuwa hakuwa na makosa ya wizi na ghasia, na hivyo hukumu yake kufutwa mwezi Machi.Moore alikuwa amesitisha kucheza katika WNBA mwaka 2019 ili aweze kuhakikisha anaachiliwa huru.“Tulioana miezi kadhaa iliyopita na tunafurahia kuendelea na ukurasa huu mpya wa maisha pamoja,” Moore mwenye umri wa miaka 31, alikiambia kipindi cha Good Morning America. Moore alichaguliwa awali katika awamu ya kwanza ya mchezo kuchezea timu yaMinnesota Lynx mnamo mwaka 2011, ambapo aliisaidia kushinda vikombe vinne  na kutangazwa kama mchezaji bora zaidi au MVP mwaka 2014.Mchezaji huyo, ambaye ni mmoja wa wachezaji bora zaidi katika historia ya WNBA pia ana medali ya dhahabu za Olimpiki na  mbili za Shindano la Dunia la mchezo huo.,

MCHEZAJI nyota wa mpira wa kikapu nchini Marekani, Maya Moore, ameolewa na Jonathan Irons mwanamme aliyemsaidia kumuondoa jela baada ya kufungwa bila hatia.

Irons aliachiliwa huru tarehe 23 Julai baada ya kufungwa  miaka 23, na baadaye kubainika kuwa hakuwa na makosa ya wizi na ghasia, na hivyo hukumu yake kufutwa mwezi Machi.

Moore alikuwa amesitisha kucheza katika WNBA mwaka 2019 ili aweze kuhakikisha anaachiliwa huru.

“Tulioana miezi kadhaa iliyopita na tunafurahia kuendelea na ukurasa huu mpya wa maisha pamoja,” Moore mwenye umri wa miaka 31, alikiambia kipindi cha Good Morning America.

 

Moore alichaguliwa awali katika awamu ya kwanza ya mchezo kuchezea timu yaMinnesota Lynx mnamo mwaka 2011, ambapo aliisaidia kushinda vikombe vinne  na kutangazwa kama mchezaji bora zaidi au MVP mwaka 2014.

Mchezaji huyo, ambaye ni mmoja wa wachezaji bora zaidi katika historia ya WNBA pia ana medali ya dhahabu za Olimpiki na  mbili za Shindano la Dunia la mchezo huo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *