Siri za mafanikio ya mtu binafsi, noreply@blogger.com (Muungwana Blog), on August 30, 2020 at 7:30 pm

August 30, 2020

Tunapoongelea suala la neno mafanikio, Kila mtu huwa ana maana yake kwa wakati wake na kwa eneo lake katika maisha. Nikiwa na maana kuwa kila mtu ana tafsiri yake kuhusu mafanikio kutokana na muda na wakati alionao na anaoendelea kuuishi hapa duniani.Kwani kuna Mafanikio mengi kutokana na mtu mwenyewe kwa muda husika anavyohitaji afanikiwe, kwa njia hiyo ndio maana huleta tafsiri halisi ya yeye kuelewa kile anachotaka kufanikiwa kwa wakati huo aliokuwa nao.Kuna mafanikio ya kiafya, kuna mafanikio ya kiuchumi na kifedha na kuna mafanikio ya uhusiano mzuri nk. Yote hayo na mengine mengi ni sehemu mojawapo ya maeneo ambayo kila mtu huhitaji kufanikiwa kutokana na kipindi na muda husika alionao duniani.Katika makala yetu hii nitazungumzia zaidi juu ya mafanikio ya kiuchumi na kifedha, hasa kwa mtu binafsi anayehitaji kuishi akiwa na uhuru wa kifedha na uchumi katika maisha yake hapa duniani.Zipo siri nyingi ninazoweza kukupa na zikakusaidia kufanikiwa katika eneo hili la uchumi na fedha, lakini ndani ya makala yetu nitazungumzia juu ya siri saba muhimu ambazo ndio ngunzo kuu ya kukusaidia kufikia mafanikio makubwa ya kiuchumi na kifedha, na hata katika maeneo mengine ya maisha yako kama vile afya, uhusiano nk. hutumika pia.Hivyo ni muhimu kuishi maisha ya mafanikio iwe katika suala la uchumi na fedha, uhusiano, imani na afya. Kwa kuzingatia jambo hilo ni muhimu uzingatie kanuni na siri zifuatazo:Imani na Ibada.Katika jambo lililo la muhimu na kipekee ambalo mtu yoyote anayehitaji kufanikiwa katika maisha yake anapaswa kulifanya; kati ya mambo yote saba nitakayozungumzia hapa, hili la imani na ibada ni la muhimu sana na ni vyema niseme linafaa kuwa la lazima kufanywa kila mara na mtu anayehitaji mafanikio makubwa maishani mwake.Hakuna njia ya kufanikiwa pasipo uhusiano wa imani na ibada. Ndio maana wapo watu wanaoenda kwa waganga wa kienyeji kwa ajili ya kupata mali na utajiri wanaohitaji, na wapo wanaomwamini Mwenyezi Mungu kama ndiye msaada wao katika maisha ya kufanikiwa kwao.Yote kwa yote katika hayo sawa na unavyoamini la muhimu kwangu kukufahamisha katika hili ni kwamba; ni vyema uwe na imani na ibada katika kile unachokiamini ili uweze kupata baraka na mafanikio ya kweli maishani mwako. Hasa Mwamini Mwenyezi Mungu, zaidi ya vitu vingine vya kupita.Jifunze kuwa na ibada kila mara na tambua binadamu si kazi ya mikono yetu binafsi, bali ni kazi iliyotokana na Mungu mwenyezi mwenyewe na kila mwanadamu ana fungu lake jema mbele ya Mwenyezi Mungu aliyemuumba.Kufanya Kazi kwa bidii.Suala nzima la kufanikiwa katika maisha linahitaji kujitoa na kujikana kila mara iitwapo leo ili kuhakikisha unafanikiwa na kuwa na mwelekeo mzuri na mwema wa kimaisha.Kufanya kazi kwa bidii huendana na ufanisi na ujuzi wako ulionao, ambavyo katika vyote hivyo pamoja ukizingatia vitaleta matokeo chanya na ya tofauti katika ulimwengu wako wa uhitaji wa mafanikio yako.Acha kuwa mtu wa malalamiko na kukata tamaa kwa haraka, bali anza kuanzia sasa kujituma na kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza kipato chako cha kila siku unachohitaji maishani.Kuwa Msomaji zaidi.Kusoma mambo mbali mbali yahusuyo maisha na yanayohusu kile kitu ulichowekeza maishani mwako kukifanya; hiyo ni sehemu tosha inayoweza kukubadilisha fikra zako na kukufanya kuwa bora, mtaalamu na mfanisi mkubwa katika utafutaji wa mafanikio yako.Hivyo basi unahitaji kuwa msomaji zaidi wa masuala mbali mbali yanayogusa eneo la Maisha yako, mafanikio yako na uchumi wako kiujumla; ili kukupa ujuzi na utaalamu mkubwa wa namna ya kufanya.Tambua ninapozungumzia suala la kusoma sina maana ya kwamba unatakiwa uingie darasani tu, HAPANA. Hapa nina maana kwamba ujifunze kusoma mambo hata yale ya kawaida kabisa yahusuyo maisha ya mafanikio yako binafsi zaidi.Kama vile ulivyotoa muda wako kwa wakati huu kusoma makala hii katika mtandao huu, hakikisha tabia hii uliyoianza isiondoke kwako kabisa bali uiendeleze kwa bidii na juhudi kubwa kila siku maishani mwako.Anza kusoma vitabu mbali mbali vinavyohusu na kuongelea maendeleo ya mtu binafsi, utajiri, kuwekeza, afya, usafi, ufanisi wa kazi, masoko nk. vitabu kama vile Self Made Millionare, Rich Dad Poor Dad, Maximum Achievement, The power of positive thinking nk.Tembelea mitandao mbali mbali yenye kutoa elimu na mafunzo mbali mbali ya kibiashara, maendeleo ya mtu binafsi, utajiri na kuwekeza nk. Mitandao kama vile huu wa WhatsAp, facebook na mingine mingi iliyopo kwa sasa.Uhusiano Mzuri na watu.Katika dunia ya leo kama unahitaji kufikia mafanikio makubwa zaidi maishani mwako, hili ndio jambo au siri muhimu unayopaswa kuitekeleza haraka na kuizingatia kwa umakini mkubwa.Kuwa na uhusiano mzuri na watu wa karibu yako ulionao ni jambo jema linaloweza kukuweka katika mazingira mazuri zaidi ya mafanikio makubwa na ukawa mtu wa tofauti na wengine katika nyanja zote za kimaisha.Kama ukikosa uhusiano mzuri na watu kuna athari kubwa ya kukosa furaha na amani; na kama ukikosa furaha na amani kuna athari kubwa pia ya kukosa uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi na bidii, kwa sababu umekosa furaha inayokufanya uwe mwenye amani katika mazingira ya kazi na watu wenyewe kiujumla.Kuwa na Nidhamu ya Muda.Hili ni jambo ambalo watu wengi wa jamii yetu tuliyonayo wameshindwa kulifanikisha kwa asilimia kubwa katika mazingira yao yote ya kimaisha na kazi, hivyo limesababisha watu wengi kushindwa kufikia malengo makubwa na mazuri waliojiwekea maishani mwao.Nataka nikuambie muda ndio msingi mzuri na wa kipekee wa kukusaidia kufikia malengo yote ya kwako uliojiwekea na unayotaka yafanikiwe katika maisha yako hapa duniani.Huwezi kufikia mafanikio makubwa na kufanikisha malengo yako kama bado hauna nidhamu ya kutosha ya kutunza muda ulionao kila siku.Jifunze kwenda na muda ili uongeze ubora wako, heshima yako na nidhamu yako binafsi katika maisha yako na eneo la kazi kiujumla kila siku.Nidhamu ya Matumizi ya Fedha.Suala la kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha limenenwa sana na watu wengi katika dunia ya leo. Waandishi wengi wa vitabu vya kibiashara na maendeleo ya mtu binafsi wamejaribu kulisema na kulielezea jambo hili kwa ufanisi katika vitabu vyao mbali mbali walivyovitoa.Nami kwa makala yangu niliyowahi kutoa katika mtandao wetu mahali hapa CICBAT, niliwahi kuzungumzia juu ya suala hili la matumizi ya fedha. Hebu kwa kujifunza zaidi juu ya eneo hili ni vyema usome makala hii; Fanya hivi kama unataka kufanikiwa katika matumizi mazuri ya fedha zako.Ni vizuri usome makala hiyo ya matumizi ya fedha baada ya kumaliza kusoma makala hii nzuri uliyokwisha kuanza kuisoma tangu hapo kwanza.Kujiamini na Kujikubali binafsi.Ni moja ya siri kubwa ambayo watu wengi hawajaitambua na wengine kuitambua lakini kutoitilia maanani katika utekelezaji wake.Kujiamini ni hali pekee ndani ya mtu ya kuwa jasiri bila uogo katika jambo lolote lile analolikabili mbele yake. Huku kujikubali pia ni sehemu muhimu inayomfanya mtu kujiona wa tofauti na wa kipekee katika mazingira ya kile anachokifanya au kutaka kukifanya.Hivyo tambua mambo yote hayo mawili yanaenda pamoja pasipo jambo moja kuacha jingine. Ni vyema kabisa uwe na tabia ya kujifunza kujiamini na kujikubali kama kweli unahitaji kufanikiwa na kufikia maono na malengo yako makubwa uliyonayo hapa duniani.Huwezi kufanikiwa kamwe kama hauna tabia ya kujiamini na kujikubali katika jambo lolote unalotaka kulifanya au unalolifanya. Tabia hizi mbili huleta tabia nyingine ya UTHUBUTU yaani tabia ya kujaribu kufanya mambo na huondoa uoga ndani ya mtu.Katika kufahamu jambo hili zaidi hebu soma makala hii; Sababu moja ni hii, kwa nini hadi sasa umeshindwa kuanza biashara.Hizo ndio siri muhimu za maisha ya mafanikio ya mtu binafsi hasa kwa yale anayohitaji. Ushauri wangu kwako ni muhimu kila unaposoma makala moja kama hii ujifunze kuweka kwenye matendo haraka (immediate) yale yote uliyoyasoma mahali hapa.Kwa kufanya hivyo itakusaidia zaidi kufanikiwa haraka katika malengo na mipango yako yote uliyojiwekea maishani mwako.,

Tunapoongelea suala la neno mafanikio, Kila mtu huwa ana maana yake kwa wakati wake na kwa eneo lake katika maisha. Nikiwa na maana kuwa kila mtu ana tafsiri yake kuhusu mafanikio kutokana na muda na wakati alionao na anaoendelea kuuishi hapa duniani.

Kwani kuna Mafanikio mengi kutokana na mtu mwenyewe kwa muda husika anavyohitaji afanikiwe, kwa njia hiyo ndio maana huleta tafsiri halisi ya yeye kuelewa kile anachotaka kufanikiwa kwa wakati huo aliokuwa nao.

Kuna mafanikio ya kiafya, kuna mafanikio ya kiuchumi na kifedha na kuna mafanikio ya uhusiano mzuri nk. Yote hayo na mengine mengi ni sehemu mojawapo ya maeneo ambayo kila mtu huhitaji kufanikiwa kutokana na kipindi na muda husika alionao duniani.

Katika makala yetu hii nitazungumzia zaidi juu ya mafanikio ya kiuchumi na kifedha, hasa kwa mtu binafsi anayehitaji kuishi akiwa na uhuru wa kifedha na uchumi katika maisha yake hapa duniani.

Zipo siri nyingi ninazoweza kukupa na zikakusaidia kufanikiwa katika eneo hili la uchumi na fedha, lakini ndani ya makala yetu nitazungumzia juu ya siri saba muhimu ambazo ndio ngunzo kuu ya kukusaidia kufikia mafanikio makubwa ya kiuchumi na kifedha, na hata katika maeneo mengine ya maisha yako kama vile afya, uhusiano nk. hutumika pia.

Hivyo ni muhimu kuishi maisha ya mafanikio iwe katika suala la uchumi na fedha, uhusiano, imani na afya. Kwa kuzingatia jambo hilo ni muhimu uzingatie kanuni na siri zifuatazo:

Imani na Ibada.
Katika jambo lililo la muhimu na kipekee ambalo mtu yoyote anayehitaji kufanikiwa katika maisha yake anapaswa kulifanya; kati ya mambo yote saba nitakayozungumzia hapa, hili la imani na ibada ni la muhimu sana na ni vyema niseme linafaa kuwa la lazima kufanywa kila mara na mtu anayehitaji mafanikio makubwa maishani mwake.

Hakuna njia ya kufanikiwa pasipo uhusiano wa imani na ibada. Ndio maana wapo watu wanaoenda kwa waganga wa kienyeji kwa ajili ya kupata mali na utajiri wanaohitaji, na wapo wanaomwamini Mwenyezi Mungu kama ndiye msaada wao katika maisha ya kufanikiwa kwao.

Yote kwa yote katika hayo sawa na unavyoamini la muhimu kwangu kukufahamisha katika hili ni kwamba; ni vyema uwe na imani na ibada katika kile unachokiamini ili uweze kupata baraka na mafanikio ya kweli maishani mwako. Hasa Mwamini Mwenyezi Mungu, zaidi ya vitu vingine vya kupita.

Jifunze kuwa na ibada kila mara na tambua binadamu si kazi ya mikono yetu binafsi, bali ni kazi iliyotokana na Mungu mwenyezi mwenyewe na kila mwanadamu ana fungu lake jema mbele ya Mwenyezi Mungu aliyemuumba.

Kufanya Kazi kwa bidii.
Suala nzima la kufanikiwa katika maisha linahitaji kujitoa na kujikana kila mara iitwapo leo ili kuhakikisha unafanikiwa na kuwa na mwelekeo mzuri na mwema wa kimaisha.
Kufanya kazi kwa bidii huendana na ufanisi na ujuzi wako ulionao, ambavyo katika vyote hivyo pamoja ukizingatia vitaleta matokeo chanya na ya tofauti katika ulimwengu wako wa uhitaji wa mafanikio yako.

Acha kuwa mtu wa malalamiko na kukata tamaa kwa haraka, bali anza kuanzia sasa kujituma na kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza kipato chako cha kila siku unachohitaji maishani.

Kuwa Msomaji zaidi.
Kusoma mambo mbali mbali yahusuyo maisha na yanayohusu kile kitu ulichowekeza maishani mwako kukifanya; hiyo ni sehemu tosha inayoweza kukubadilisha fikra zako na kukufanya kuwa bora, mtaalamu na mfanisi mkubwa katika utafutaji wa mafanikio yako.
Hivyo basi unahitaji kuwa msomaji zaidi wa masuala mbali mbali yanayogusa eneo la Maisha yako, mafanikio yako na uchumi wako kiujumla; ili kukupa ujuzi na utaalamu mkubwa wa namna ya kufanya.

Tambua ninapozungumzia suala la kusoma sina maana ya kwamba unatakiwa uingie darasani tu, HAPANA. Hapa nina maana kwamba ujifunze kusoma mambo hata yale ya kawaida kabisa yahusuyo maisha ya mafanikio yako binafsi zaidi.

Kama vile ulivyotoa muda wako kwa wakati huu kusoma makala hii katika mtandao huu, hakikisha tabia hii uliyoianza isiondoke kwako kabisa bali uiendeleze kwa bidii na juhudi kubwa kila siku maishani mwako.

Anza kusoma vitabu mbali mbali vinavyohusu na kuongelea maendeleo ya mtu binafsi, utajiri, kuwekeza, afya, usafi, ufanisi wa kazi, masoko nk. vitabu kama vile Self Made Millionare, Rich Dad Poor Dad, Maximum Achievement, The power of positive thinking nk.
Tembelea mitandao mbali mbali yenye kutoa elimu na mafunzo mbali mbali ya kibiashara, maendeleo ya mtu binafsi, utajiri na kuwekeza nk. Mitandao kama vile huu wa WhatsAp, facebook na mingine mingi iliyopo kwa sasa.

Uhusiano Mzuri na watu.
Katika dunia ya leo kama unahitaji kufikia mafanikio makubwa zaidi maishani mwako, hili ndio jambo au siri muhimu unayopaswa kuitekeleza haraka na kuizingatia kwa umakini mkubwa.

Kuwa na uhusiano mzuri na watu wa karibu yako ulionao ni jambo jema linaloweza kukuweka katika mazingira mazuri zaidi ya mafanikio makubwa na ukawa mtu wa tofauti na wengine katika nyanja zote za kimaisha.

Kama ukikosa uhusiano mzuri na watu kuna athari kubwa ya kukosa furaha na amani; na kama ukikosa furaha na amani kuna athari kubwa pia ya kukosa uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi na bidii, kwa sababu umekosa furaha inayokufanya uwe mwenye amani katika mazingira ya kazi na watu wenyewe kiujumla.

Kuwa na Nidhamu ya Muda.
Hili ni jambo ambalo watu wengi wa jamii yetu tuliyonayo wameshindwa kulifanikisha kwa asilimia kubwa katika mazingira yao yote ya kimaisha na kazi, hivyo limesababisha watu wengi kushindwa kufikia malengo makubwa na mazuri waliojiwekea maishani mwao.

Nataka nikuambie muda ndio msingi mzuri na wa kipekee wa kukusaidia kufikia malengo yote ya kwako uliojiwekea na unayotaka yafanikiwe katika maisha yako hapa duniani.
Huwezi kufikia mafanikio makubwa na kufanikisha malengo yako kama bado hauna nidhamu ya kutosha ya kutunza muda ulionao kila siku.

Jifunze kwenda na muda ili uongeze ubora wako, heshima yako na nidhamu yako binafsi katika maisha yako na eneo la kazi kiujumla kila siku.

Nidhamu ya Matumizi ya Fedha.
Suala la kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha limenenwa sana na watu wengi katika dunia ya leo. Waandishi wengi wa vitabu vya kibiashara na maendeleo ya mtu binafsi wamejaribu kulisema na kulielezea jambo hili kwa ufanisi katika vitabu vyao mbali mbali walivyovitoa.

Nami kwa makala yangu niliyowahi kutoa katika mtandao wetu mahali hapa CICBAT, niliwahi kuzungumzia juu ya suala hili la matumizi ya fedha. Hebu kwa kujifunza zaidi juu ya eneo hili ni vyema usome makala hii; Fanya hivi kama unataka kufanikiwa katika matumizi mazuri ya fedha zako.

Ni vizuri usome makala hiyo ya matumizi ya fedha baada ya kumaliza kusoma makala hii nzuri uliyokwisha kuanza kuisoma tangu hapo kwanza.

Kujiamini na Kujikubali binafsi.
Ni moja ya siri kubwa ambayo watu wengi hawajaitambua na wengine kuitambua lakini kutoitilia maanani katika utekelezaji wake.

Kujiamini ni hali pekee ndani ya mtu ya kuwa jasiri bila uogo katika jambo lolote lile analolikabili mbele yake. Huku kujikubali pia ni sehemu muhimu inayomfanya mtu kujiona wa tofauti na wa kipekee katika mazingira ya kile anachokifanya au kutaka kukifanya.

Hivyo tambua mambo yote hayo mawili yanaenda pamoja pasipo jambo moja kuacha jingine. Ni vyema kabisa uwe na tabia ya kujifunza kujiamini na kujikubali kama kweli unahitaji kufanikiwa na kufikia maono na malengo yako makubwa uliyonayo hapa duniani.

Huwezi kufanikiwa kamwe kama hauna tabia ya kujiamini na kujikubali katika jambo lolote unalotaka kulifanya au unalolifanya. Tabia hizi mbili huleta tabia nyingine ya UTHUBUTU yaani tabia ya kujaribu kufanya mambo na huondoa uoga ndani ya mtu.

Katika kufahamu jambo hili zaidi hebu soma makala hii; Sababu moja ni hii, kwa nini hadi sasa umeshindwa kuanza biashara.

Hizo ndio siri muhimu za maisha ya mafanikio ya mtu binafsi hasa kwa yale anayohitaji. Ushauri wangu kwako ni muhimu kila unaposoma makala moja kama hii ujifunze kuweka kwenye matendo haraka (immediate) yale yote uliyoyasoma mahali hapa.

Kwa kufanya hivyo itakusaidia zaidi kufanikiwa haraka katika malengo na mipango yako yote uliyojiwekea maishani mwako.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *