Simulizi ya mwanamume wa Rwanda anayetaka kuoa wanawake 11, on September 19, 2020 at 6:00 pm

September 19, 2020

 Salongo Mayanja(Maniraguha) ni mganga wa kienyeji nchini Rwanda ambaye ameamua kufuata nyayo za baba yake kwa kuoa wanawake wengi.Kwa sasa bwana Salongo Mayanja ana wake wanane na anasema anataka kuwa na wanawake 11 kama bab yake mzazi.Anasema kuoa wanawake wengi ”ni raha isiyo na kifani ukiwa na uwezo kifedha”.Pengine huenda unajiuliza anamudu vipi kutatua tofauti za kawaida zinazohusishwa na wake wenza?Kujibu swali hilo na maswali mengine mengi mwandishi wa BBC Yves Bucyana alimtembelea Salongo Mayanja katika moja ya nyumba zake mjini Musanze kaskazini mwa Rwanda na kutuandalia makala haya.Mara kwa mara bwana Salongo huwakutanisha wake zake wanane ili kama njia ya kudumisha upendo kati yao.”Hii ni siku maalumu isiyo ya kawaida kwa sababu wake wenza nimewatayarishia zawadi kwa ukarimu walionionesha” alisema.Siku hiyo maalum kila mke anaonekana mwenye furaha. Mmoja wao ambaye ndiye mke mdogo, aliolewa na Salongo wiki mbili zilizopita”Nilikuwa na mchumba mwengine.Lakini mwishowe nilimkatia na kukubali kuolewa na huyu Bwana licha ya kwamba nilijua ana wake wengine wengi” anamsimulia mwandishi wa BBC.Familia ya bwana Salonga hujumuika kila baada ya miezi mitatu kwa mwaliko wake ambapo wanasherehekea pamoja na kupeana zawadi.Wakati baadhi ya watu wanaona kwamba ni mzigo mkubwa kuoa na kutunza zaidi ya mke mmoja kutokana na hali ya maisha inavyozidi kuwa ngumu,Lakini yeye anasema kuishi na wake wengi ni raha.”Naishi nao vizuri kuliko mtu aliye na mke mmoja ambapo unakuta wanaishi kwa ugomvi usiokwisha”Pia anaongezea kusema kuwa anasaidia serikali kutunza hawa wanawake sababu kila mke wangu niliyemuoa ”anasaidia pia familia yake yote” kwasababu ana uwezo.”Kila mwanamke ana shamba nanyumba yake kiasi kwa hatahangaika yeye na watoto wake mimi nitakapokuwa sipo” aliendelea kusema kwa madaha.Wake zake wenyewe wanasema wanaishi pamoja vizuri bila mtafaruku wowote wala wivu kama anavyosimulia mmoja wao Uwanyirigira Jeanne D’Arc.,

 

Salongo Mayanja(Maniraguha) ni mganga wa kienyeji nchini Rwanda ambaye ameamua kufuata nyayo za baba yake kwa kuoa wanawake wengi.

Kwa sasa bwana Salongo Mayanja ana wake wanane na anasema anataka kuwa na wanawake 11 kama bab yake mzazi.

Anasema kuoa wanawake wengi ”ni raha isiyo na kifani ukiwa na uwezo kifedha”.

Pengine huenda unajiuliza anamudu vipi kutatua tofauti za kawaida zinazohusishwa na wake wenza?

Kujibu swali hilo na maswali mengine mengi mwandishi wa BBC Yves Bucyana alimtembelea Salongo Mayanja katika moja ya nyumba zake mjini Musanze kaskazini mwa Rwanda na kutuandalia makala haya.

Mara kwa mara bwana Salongo huwakutanisha wake zake wanane ili kama njia ya kudumisha upendo kati yao.

”Hii ni siku maalumu isiyo ya kawaida kwa sababu wake wenza nimewatayarishia zawadi kwa ukarimu walionionesha” alisema.

Siku hiyo maalum kila mke anaonekana mwenye furaha. Mmoja wao ambaye ndiye mke mdogo, aliolewa na Salongo wiki mbili zilizopita

”Nilikuwa na mchumba mwengine.Lakini mwishowe nilimkatia na kukubali kuolewa na huyu Bwana licha ya kwamba nilijua ana wake wengine wengi” anamsimulia mwandishi wa BBC.

Familia ya bwana Salonga hujumuika kila baada ya miezi mitatu kwa mwaliko wake ambapo wanasherehekea pamoja na kupeana zawadi.

Wakati baadhi ya watu wanaona kwamba ni mzigo mkubwa kuoa na kutunza zaidi ya mke mmoja kutokana na hali ya maisha inavyozidi kuwa ngumu,Lakini yeye anasema kuishi na wake wengi ni raha.

”Naishi nao vizuri kuliko mtu aliye na mke mmoja ambapo unakuta wanaishi kwa ugomvi usiokwisha”

Pia anaongezea kusema kuwa anasaidia serikali kutunza hawa wanawake sababu kila mke wangu niliyemuoa ”anasaidia pia familia yake yote” kwasababu ana uwezo.

”Kila mwanamke ana shamba nanyumba yake kiasi kwa hatahangaika yeye na watoto wake mimi nitakapokuwa sipo” aliendelea kusema kwa madaha.

Wake zake wenyewe wanasema wanaishi pamoja vizuri bila mtafaruku wowote wala wivu kama anavyosimulia mmoja wao Uwanyirigira Jeanne D’Arc.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *