Simba yaweka Rekodi Mpya, noreply@blogger.com (Udaku Special)

August 31, 2020

Klabu ya Simba ilifanikiwa kutwaa Ubingwa wa Ngao ya Jamii baada ya hapo jana kuifunga Namungo kwa bao mbili kwa sifuri katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha na kuweka rekodi mbali mbali.Klabu ya Simba ikishangilia baada ya kutwaa taji la Ngao ya Jamii msimu uliopita.Ushindi katika mchezo wa jana wa Ngao ya jamii wa Simba Sc dhidi ya Namungo Fc umewafanya wekundu wa msimbazi kuandika historia ya kutwaa taji la michuano hiyo mara nyingi zaidi ikiwa imefanya mara sita.Simba Sc kabla ya jana ilichukua taji hilo mwaka 2011, 2012,2017, 2018 na 2019 sawa na watani wao Yanga ambao wenyewe walichukua mwaka 2001, 2010, 2013, 2014 na 2015.Ushindi wa jana wa mabao mawili kwa sifuri yaliyofungwa na Nahodha wake John Bocco kwa penati na Benard Morrison,liliwafanya watwae taji la sita.Pia Simba iliandika rekodi ya kuwa timu iliyotwaa Ngao ya Jamii mara nyingi mfululizo ambapo ilifanya kwa mara ya nne.Kwa upande wa Namungo, iwapo wangepata ushindi ingekua timu ya kwanza kutoka Kanda ya Kusini ambayo ilishiriki ligi kwa msimu mmoja tu Ligi Kuu.,

Klabu ya Simba ilifanikiwa kutwaa Ubingwa wa Ngao ya Jamii baada ya hapo jana kuifunga Namungo kwa bao mbili kwa sifuri katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha na kuweka rekodi mbali mbali.

Klabu ya Simba ikishangilia baada ya kutwaa taji la Ngao ya Jamii msimu uliopita.

Ushindi katika mchezo wa jana wa Ngao ya jamii wa Simba Sc dhidi ya Namungo Fc umewafanya wekundu wa msimbazi kuandika historia ya kutwaa taji la michuano hiyo mara nyingi zaidi ikiwa imefanya mara sita.

Simba Sc kabla ya jana ilichukua taji hilo mwaka 2011, 2012,2017, 2018 na 2019 sawa na watani wao Yanga ambao wenyewe walichukua mwaka 2001, 2010, 2013, 2014 na 2015.

Ushindi wa jana wa mabao mawili kwa sifuri yaliyofungwa na Nahodha wake John Bocco kwa penati na Benard Morrison,liliwafanya watwae taji la sita.

Pia Simba iliandika rekodi ya kuwa timu iliyotwaa Ngao ya Jamii mara nyingi mfululizo ambapo ilifanya kwa mara ya nne.

Kwa upande wa Namungo, iwapo wangepata ushindi ingekua timu ya kwanza kutoka Kanda ya Kusini ambayo ilishiriki ligi kwa msimu mmoja tu Ligi Kuu.,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *