Simba, Azam zatua Mbeya kwa kishindo,

October 19, 2020

Klabu za Simba na Azam zimewasili jijini Mbeya ikiwa ni katika matayarisho ya mechi zao ligi kuu Tanzania bara zitakazochezwa katikati ya wiki hii.

Azam watakua wageni wa Ihefu ambayo inahaha kujiondoa katika nafasi za chini ya msimamo, huku ikitarajiwa kuongozwa na Zuberi Katwila ambaye jana alitangazwa kuwa ndiye mrithi wa Maka Mwalwisi aliyetimuliwa hivi karibuni.

Wanalambalamba wao wanawania ushindi wa saba mfululizo katika VPL ili iendelee kujikita kileleni wa ligi iwapo watashinda mchezo wa kesho utakaochezwa kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.

Kwa upande wa mabingwa watetezi, Simba wamewasili jijini Mbeya ambapo wataweka kambi ya siku mbili kabla ya kuelekea Rukwa ambapo itakabiliana na Tanzania Prisons Oktoba 22 mwaka huu.

Kikosi cha Simba kitaikabili Prisons bila ya uwepo wa mshambuliaji wake kinara Meddie Kagere ambaye atakua nje ya dimba kwa wiki tatu kufuatia majeruhi aliyoyapata akiwa katika timu yake ya taifa ya Rwanda.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *