Shirika la umma la jamii ya Waislamu lavamiwa na polisi Ufaransa,

October 15, 2020

 

Maafisa wa polisi wa Ufaransa wameripotiwa kuvamia shirika la umma la jamii ya Waislamu la Baraka City.

Mashirika ya umma ya jamii ya Waislamu yaliyokuwa ndani ya mji mkuu wa Paris nchini Ufaransa, yamekuwa yakikumbwa na uvamizi katika wiki za hivi karibuni.

Mara ya mwisho shirika la umma la jamii ya Waislamu la Baraka City limeripotiwa kuvamiwa na maafisa wa polisi.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolea kwenye mtandao wa kijamii kupitia akaunti ya Baraka City, nyumba ya mwanzilishi wa shirika hilo Idris Sihamedi pia imeripotiwa kuvamiwa.

Sihamedi alitiwa mbaroni na maafisa wa polisi mbele ya watoto wake.

Maafisa wa polisi pia walimfunga pingu mkewe Sihamedi, na kuwaamuru watoto wake waweke mikono hewani.

Mamlaka za Ufaransa hazijatoa maelezo yoyote kuhusu tukio hilo.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Gerard Darmanin, alimshutumu Idris Sihamedi kwa madai ya kuunda mkono ugaidi.

Hapo awali, shirika la Baraka City pia liliwahi kusimamishwa kwa madai ya ugaidi.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *