Shirika la Ndege la Uganda larudisha safari zake nchini Tanzania

October 3, 2020

Viongozi wa Ubalozi wa Uganda nchini Tanzania, Wafanyakazi wa Shirika la ndege la Uganda wa Tanzania na Uganda, abiria wa waliokuja na ndege hiyo pamoja na maofisa wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Terminal III wakifurahia mara baada ya ndege ya shirika hilo kuwasili nchini Tanzania kwa mara ya kwanza baada janga la Virusi vya Corona kupungua kwa kiasi kikubwa.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la ndege la Uganda Ahabwe Godfrey Pereza(katikati) akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la ndege la Uganda wa Tanzania pamoja na wa Uganda, viongozi wa Uwanja wa ndege wa JNIA pamoja na waandishi wa habari mara baada ya ndege ya shirika hilo aina ya Bombardier CRJ900 kuwasiri kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa mara ya kwanza baada ya Virusi vya Corona kupungua katika nchi mbalimbali. Kushotoni Mwakilishi wa Ubalozi wa Uganda nchini Musekura Eseza na kushoto ni Meneja Biashara Shirika la ndege la Uganda Roger Wamara

Meneja Biashara Shirika la ndege la Uganda Roger Wamara akizungumza Shirika la ndege la Uganda wa Tanzania pamoja na wa Uganda, viongozi wa Uwanja wa ndege wa JNIA pamoja na waandishi wa habari kuhusu namna walivyojipanga kuweza kurudisha afari kama ilivyokuwa mwanzo kabla ya kutokea janga la Virusi vya Corona vilivyopelekea kusitishwa kwa ndege za shirika hilo. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Jengo la Terminal III katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) .

Viongozi wa Ubalozi wa Uganda nchini Tanzania, Wafanyakazi wa Shirika la ndege la Uganda wa Tanzania na Uganda pamoja na maofisa wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Terminal III wakifurahia kuanza kwa safari za ndege ya Shirika la ndege la Uganda mara baada ya ndege hiyo kuwasili katika uwanja huo kwa mara ya kwanza tokea janga la Virusi vya Corona limezikumba nchi nyingi Duniani ikiwemo Tanzania.

 Ndege ya Shirika la ndege la Uganda aina ya Bombardier CRJ900 ikiwa imewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ikitokea nchini Uganda kwa mara ya kwanza baada ya janga la Virusi vya Corona lililoikumba Dunia.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *