Shamsa Ford aacha wosia mzito

October 17, 2020

 

Msanii wa filamu Shamsa Ford amechia ujumbe mzito kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kwa kuwataka mashabiki wasipende kuwahukumu watu maarufu kwa makosa yao kwani nao ni binaadam wanapitiwa kama inavyotokea kwa watu wengine.

Shamsa Ford amesema kuna watu wakiwaona mastaa mitandaoni wanahisi ni tofauti na walivyo wao ndiyo maana wanawakuhumiwa  kwa kuwashambulia na matusi pale wanapokosea.

“Wengine wakituona kwenye mitandao wanatuhukumu tofauti, sisi ni binadamu kama nyie saa nyingine tunapitiwa kama binadamu wengine kwasababu hakuna mwanadamu aliyekamilika zaidi ya  Mungu ila maisha yetu pia huwa tunaishi kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu, tusijisahau sana na dunia” 

“Kulikuwa na matajiri wengi, wazuri wengi, watu maarufu wengi lakini leo hii hatupo nao duniani, tuishi kwa kuthaminiana epuka kumuumiza mwanadamu mwenzio kwa makusudi sisi sote si chochote mbele ya Mwenyezi Mungu” ameongeza 

Aidha msanii huyo amesema amekaa kimya na kudhalilishwa vya kutosha hivyo atatangaza siku ya kuwa na mkutano na waandishi wa habari ili kuzungumzia ukweli wote yanaondelea dhidi yake

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *