Shambulizi la bomu la kutegwa garini laua watu 12 Afghanistan, 100 wajeruhiwa,

October 18, 2020

 Watu wasiopungua 12 wameuawa leo kufuatia shambulizi la bomu lililotegwa garini katika jimbo la Ghor magharibi mwa Afghanistan. 

Hayo yamesemwa na maafisa ambao wameongeza kuwa zaidi ya watu wengine 100 wamejeruhiwa kwenye shambulizi hilo. 

Mkuu wa hospitali katika jimbo la Ghor Mohammad Omer Lalzad amesema wahudumu wa afya wanawapatia matibabu watu kadhaa waliopata majeraha mabaya kwenye tukio hilo. Omer ameongeza kuwa anatarajia idadi ya vifo kuongezeka. 

Msemaji wa Wizara ya mambo ya ndani Tariq Aran amesema shambulizi hilo, limefanywa karibu na lango la kuingia katika ofisi ya mkuu wa polisi wa jimbo hilo, inayopakana na majengo kadhaa ya serikali katika eneo hilo. 

Hakuna kundi ambalo limejitokeza mara moja kukiri kuhusika na shambulizi hilo la Ghor, ambalo limejiri wakati kumekuwa na ongezeko la mashambulizi ya kundi la Taliban mnamo wakati wawakilishi wa kundi hilo na maafisa wa serikali wakifanya mazungumzo ya kwanza ya ana kwa ana nchini Qatar.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *