Serikali yazionya Taasisi zinazokwamisha uwekezaji hapa nchini, on September 11, 2020 at 1:00 pm

September 11, 2020

Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.Serikali imesema haitazivumilia taasisi zinazokwamisha uwekezaji hapa nchini kwa kuwawekea mazingira magumu wawekezaji kuwekeza hapa nchini.Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughurikia Sera, uratibu na uwekezaji Dkt Dorothy Mwaluko wakati akifungua kikao kazi na taasisi mbali mbali zinazoshughurikia wawekezaji kutathmini sera za uwekezaji.Ambapo amesema bado kuna taasisi ambazo zinakuwa kikwazo kwa wawekezaji kuwekaza hapa nchini kwa kuwawekea mazingira magumu na kushindwa kuwekeza hapa nchini.”Ninyi mko getini ni wajibu wenu kuwafungulia milango wawekezaji tunataka serikali na ninyi tuongee lugha moja sio kila taasisi inakuwa na sheria zake na haishauriki inapokuwa inakinzana na nyingine” Sio mnaweka sheria ambayo hata wewe mwenyewe tukisema haya hamia huku utekeleze hiyo sera na wewe unashindwa kuitekeleza kwa namna hiyo tutakuwa hatuwawezeshi wawekezaji kuja kuwekeza” amesema Dkt Dorothy.Pia amezitaka taasisi kuacha kuwachanganya wawekezaji kwa kutofautiana katika sera na kuwataka wawe na sheria ambazo zitamuwezesha muwekezaji kuja kuwekeza.”Tunataka ukiwa Wizara ya kazi mimi nahusika na maswala ya kazi, mimi niko uhamiaji nahusika na maswala ya uhamiaji na hivi tunahomonize namna gani?”Ili wawekezaji wakija wakienda kazi jibu ni hilo hilo wakienda uhamiaji jibu ni hilo hilo na wasema haya ni majibu kutoka Tanzania na hali iko hivi” amesema.Aidha amesema taasisi hizo hazina uamuzi wa mwisho katika kuamua sera hizo maamuzi yapo ngazi za juu za katika serikali.Kwa upande wake mtafiti wa sheria za uwekezaji hapa nchini Dkt Saudin Mwakaje amesema katika kikao hicho wataweza kutathmini hali ya uwekezaji hapa nchini na changamoto wanazozipata Taasisi hizo katika kutekeleza sera hizo.Amesema watapitia sera mbalimbali na kuona kama zinaendana na hali ya Sasa na kuma kutakuwa na uhitaji watakuja na mapendekezo ya kuzibadili sera hizo ili ziendane na wakati wa sasa.” Tunasera ambayo ilipitishwa mwaka 1996 ndio tutaijadili utekelezaji wake tunajua kuna mabadiliko mengi ya sheria ambayo yanaathiri utekelezaji wa sera za uwekezaji hivyo tutajadili mafanikio na changamoto kuboresha sera hizo” amesema Dkt Mwakaje.,

Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.

Serikali imesema haitazivumilia taasisi zinazokwamisha uwekezaji hapa nchini kwa kuwawekea mazingira magumu wawekezaji kuwekeza hapa nchini.

Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughurikia Sera, uratibu na uwekezaji Dkt Dorothy Mwaluko wakati akifungua kikao kazi na taasisi mbali mbali zinazoshughurikia wawekezaji kutathmini sera za uwekezaji.

Ambapo amesema bado kuna taasisi ambazo zinakuwa kikwazo kwa wawekezaji kuwekaza hapa nchini kwa kuwawekea mazingira magumu na kushindwa kuwekeza hapa nchini.

“Ninyi mko getini ni wajibu wenu kuwafungulia milango wawekezaji tunataka serikali na ninyi tuongee lugha moja sio kila taasisi inakuwa na sheria zake na haishauriki inapokuwa inakinzana na nyingine

” Sio mnaweka sheria ambayo hata wewe mwenyewe tukisema haya hamia huku utekeleze hiyo sera na wewe unashindwa kuitekeleza kwa namna hiyo tutakuwa hatuwawezeshi wawekezaji kuja kuwekeza” amesema Dkt Dorothy.

Pia amezitaka taasisi kuacha kuwachanganya wawekezaji kwa kutofautiana katika sera na kuwataka wawe na sheria ambazo zitamuwezesha muwekezaji kuja kuwekeza.

“Tunataka ukiwa Wizara ya kazi mimi nahusika na maswala ya kazi, mimi niko uhamiaji nahusika na maswala ya uhamiaji na hivi tunahomonize namna gani?

“Ili wawekezaji wakija wakienda kazi jibu ni hilo hilo wakienda uhamiaji jibu ni hilo hilo na wasema haya ni majibu kutoka Tanzania na hali iko hivi” amesema.

Aidha amesema taasisi hizo hazina uamuzi wa mwisho katika kuamua sera hizo maamuzi yapo ngazi za juu za katika serikali.

Kwa upande wake mtafiti wa sheria za uwekezaji hapa nchini Dkt Saudin Mwakaje amesema katika kikao hicho wataweza kutathmini hali ya uwekezaji hapa nchini na changamoto wanazozipata Taasisi hizo katika kutekeleza sera hizo.

Amesema watapitia sera mbalimbali na kuona kama zinaendana na hali ya Sasa na kuma kutakuwa na uhitaji watakuja na mapendekezo ya kuzibadili sera hizo ili ziendane na wakati wa sasa.

” Tunasera ambayo ilipitishwa mwaka 1996 ndio tutaijadili utekelezaji wake tunajua kuna mabadiliko mengi ya sheria ambayo yanaathiri utekelezaji wa sera za uwekezaji hivyo tutajadili mafanikio na changamoto kuboresha sera hizo” amesema Dkt Mwakaje.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *