Serikali yazindua Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha wa miaka 10, on September 17, 2020 at 3:00 pm

September 17, 2020

 Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.Serikali kupitia wizara ya Fedha na Mipango leo imezindua mpango  Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha utakaotumika kwa kipindi cha miaka kumi kuanzia 2020/2021 hadi 2029/2030 wenye lengo la  kuongeza wigo na fursa za upatikanaji wa huduma za fedha kwa wananchi wote zikiwemo za bima.Akizindua mpango huo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dotto James, Naibu Katibu Mkuu Mary Maganga amesema pia mpango huo utaongeza wigo katika upatikanaji wa  huduma za mikopo ,akiba ,uwekezaji na kuongeza mchango wa sekta ya fedha katika ukuaji wa uchumi unaoendeshwa na sekta ya viwanda.Pia amesema mpango huo umeandaliwa ili utumike katika kutatua changamoto zilizopo ambapo pamoja na mambo pia  umelenga kuongeza upatikanaji mitaji ya muda mrefu, upatikanaji huduma jumuishi za fedha na kulinda watumiaji wa huduma za fedha .Pia kuimarisha uthabiti wa sekta ya fedha ,kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa katika sekta ya fedha ,kudhibiti  utakatishaji fedha haramu     na kuweka mazingira wezeshi ya sheria ,kanuni ,taratibu na miongozo katika sekta ya fedha.Aidha amewataka waratibu na wasimamizi wa mpango huo kuwianisha mipango mbalimbali ili iendene na mpango huo Mkuu wa kitaifa katika maeneo wanayoyasimamia .“Maeneo hayo ni katika sekta ndogo zilizomo ndani ya sekta hii ikiwa ni pamoja na benki,bima ,masoko ya mitaji na dhamana ,mifuko ya hifadhi ya jamii na sekta ya huduma ndogo za fedha.”amesema Mary.Pia amevitaka vyuo  vikuu na taasisi za utafiti amewataka kuona fursa zilizopo katika mpango huo na kujipanga katika kuboresha maeneo mbalimbali ya kitaaluma na kiutafiti ili kuhakikisha sekta hiyo inaendelea kuwa yenye ushindani na kuweza kuhimili mabadiliko ya nyakati kwa wepesi na weledi.Kwa upande wake Kamishna wa Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha  Dkt.Charles Mwamwaja amesema wakati wa maandalizi,timu ya wataalam wa Mpango huo ilifanya mapitio kwenye nyaraka mbalimbali zikiwemo taarifa za maboresho ya sekta ya fedha ,Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025,Dira ya Taifa ya Maendeleo Zanzibar ya mwaka 2020 na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza umasikini Zanzibar (ZSGRP III) .Pia ilipitia Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa miaka mitano 2016/17-2020/21 na taarifa ya Programu ya Tathimini ya Sekta ya Fedha yam waka 2018 kwa lengo la kupata matokeo zaidi katika utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Kitaifa. ,

 

Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.
Serikali kupitia wizara ya Fedha na Mipango leo imezindua mpango  Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha utakaotumika kwa kipindi cha miaka kumi kuanzia 2020/2021 hadi 2029/2030 wenye lengo la  kuongeza wigo na fursa za upatikanaji wa huduma za fedha kwa wananchi wote zikiwemo za bima.

Akizindua mpango huo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dotto James, Naibu Katibu Mkuu Mary Maganga amesema pia mpango huo utaongeza wigo katika upatikanaji wa  huduma za mikopo ,akiba ,uwekezaji na kuongeza mchango wa sekta ya fedha katika ukuaji wa uchumi unaoendeshwa na sekta ya viwanda.

Pia amesema mpango huo umeandaliwa ili utumike katika kutatua changamoto zilizopo ambapo pamoja na mambo pia  umelenga kuongeza upatikanaji mitaji ya muda mrefu, upatikanaji huduma jumuishi za fedha na kulinda watumiaji wa huduma za fedha .

Pia kuimarisha uthabiti wa sekta ya fedha ,kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa katika sekta ya fedha ,kudhibiti  utakatishaji fedha haramu     na kuweka mazingira wezeshi ya sheria ,kanuni ,taratibu na miongozo katika sekta ya fedha.

Aidha amewataka waratibu na wasimamizi wa mpango huo kuwianisha mipango mbalimbali ili iendene na mpango huo Mkuu wa kitaifa katika maeneo wanayoyasimamia .

“Maeneo hayo ni katika sekta ndogo zilizomo ndani ya sekta hii ikiwa ni pamoja na benki,bima ,masoko ya mitaji na dhamana ,mifuko ya hifadhi ya jamii na sekta ya huduma ndogo za fedha.”amesema Mary.

Pia amevitaka vyuo  vikuu na taasisi za utafiti amewataka kuona fursa zilizopo katika mpango huo na kujipanga katika kuboresha maeneo mbalimbali ya kitaaluma na kiutafiti ili kuhakikisha sekta hiyo inaendelea kuwa yenye ushindani na kuweza kuhimili mabadiliko ya nyakati kwa wepesi na weledi.

Kwa upande wake Kamishna wa Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha  Dkt.Charles Mwamwaja amesema wakati wa maandalizi,timu ya wataalam wa Mpango huo ilifanya mapitio kwenye nyaraka mbalimbali zikiwemo taarifa za maboresho ya sekta ya fedha ,Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025,Dira ya Taifa ya Maendeleo Zanzibar ya mwaka 2020 na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza umasikini Zanzibar (ZSGRP III) .

Pia ilipitia Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa miaka mitano 2016/17-2020/21 na taarifa ya Programu ya Tathimini ya Sekta ya Fedha yam waka 2018 kwa lengo la kupata matokeo zaidi katika utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Kitaifa. 

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *