Serikali ya Ujerumani yalaani jaribio ”lisilokubalika” la kuvamia jengo la Reichstag, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 2), on August 30, 2020 at 1:00 pm

August 30, 2020

Serikali ya Ujerumani leo imelaani tabia “isiyokubalika” ya waandamanaji wakati wa maandamano dhidi ya vikwazo vya kuzuia kuenea kwa maabukizi ya virusi vya corona ambapo mamia ya watu walikamatwa na wengine kujaribu kuvamia jengo la bunge la Reichstag.Waziri wa mambo ya ndani Horst Seehofer, ameliambi gazeti la Bild katika toleo lake la Jumapili kuwa jengo hilo la Reichstag ni kituo cha ishara ya demokrasia ya nchi hiyo na kwamba haitakubalika kuwaona watu wa itikadi kali na wasumbufu wakilitumia kwa manufaa yao ya kibinafsi.Polisi inasema kuwa takriban watu elfu 38 mara mbili zaidi ya idadi iliyotarajiwa walikusanyika mjini Berlin jana Jumamosi kulalamika dhidi ya vikwazo hivyo kama vile kuvaa barakoa na kujiweka kando na watu.Hapo jana jioni, mamia ya waandamanaji walivunja vizuizi vya polisi na kupanda ngazi zilizokuwa zikielekea katika lango la jengo hilo la Reichstag.,

Serikali ya Ujerumani leo imelaani tabia “isiyokubalika” ya waandamanaji wakati wa maandamano dhidi ya vikwazo vya kuzuia kuenea kwa maabukizi ya virusi vya corona ambapo mamia ya watu walikamatwa na wengine kujaribu kuvamia jengo la bunge la Reichstag.

Waziri wa mambo ya ndani Horst Seehofer, ameliambi gazeti la Bild katika toleo lake la Jumapili kuwa jengo hilo la Reichstag ni kituo cha ishara ya demokrasia ya nchi hiyo na kwamba haitakubalika kuwaona watu wa itikadi kali na wasumbufu wakilitumia kwa manufaa yao ya kibinafsi.

Polisi inasema kuwa takriban watu elfu 38 mara mbili zaidi ya idadi iliyotarajiwa walikusanyika mjini Berlin jana Jumamosi kulalamika dhidi ya vikwazo hivyo kama vile kuvaa barakoa na kujiweka kando na watu.

Hapo jana jioni, mamia ya waandamanaji walivunja vizuizi vya polisi na kupanda ngazi zilizokuwa zikielekea katika lango la jengo hilo la Reichstag.,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *