Serikali ya Tanzania yakanusha taarifa ya Islamic State dhidi ya nchi hiyo

September 7, 2020

Huwezi kusikiliza tena

Dakika 3 zilizopita

Serikali ya Tanzania imekanusha madai yaliyotolewa na wanamgambo wa Islamic State kwamba wamewauwa ama kuwajeruhi wanajeshi wasiopungua 20 wa Tanzania wakati wakitibua shambulio kaskazini mwa Msumbiji.

Juzi Septemba 5, mtandao wa wanamgambo wa Islamic State ulidai kwamba ulitibua shambulio hilo lililotekelezwa kwa pamoja na vikosi vya Tanzania na Msumbiji katika eneo la mpakani katika mkoa wa Cabo Delgado.

Aidha taarifa hiyo ilidai kwamba wanamgambo hao walikabiliana vikali na wanajeshi wa mataifa hayo mawili, na kudai kwamba walifanikiwa kuteka silaha kadhaa, pamoja na magari manne.

Lakini msemaji wa jeshi la ulinzi Tanzania, Luteni Kanali Juma Sipe, ameiambia BBC kwamba madai hayo hayana ukweli wowote:

Source link

,Huwezi kusikiliza tena Serikali ya Tanzania yakanusha taarifa ya Islamic State dhidi ya nchi hiyo Dakika 3 zilizopita Serikali ya…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *