Serikali ya Sudan na makundi ya waasi yafikia makubaliano ya kusitisha mzozo,

October 5, 2020

Serikali ya Sudan na Chama cha Mapinduzi kilichoko magharibi na kusini mwa nchi, wamekubaliana kutian saini mkataba wa amani ili kusitisha mzozo uliokuwepo kati makundi ya waasi wenye silaha.

Hafla ya kutia saini mkataba huo wa makubaliano iliandaliwa katika mji mkuu wa Juba, Sudan Kusini, chini ya usimamizi wa Rais msaidizi wa Baraza la Sudan Jenerali Mohammed Hamdan Dakalu, mkuu wa chama cha mapinduzi Al-Hadi Idris na wajumbe wengine wa makundi ya waasi.

Viongozi wengine waliohudhuria hafla hiyo na kushuhudia makubaliano walikuwa ni Rais wa Baraza la Sudan Jenerali Abdulfettah al-Burhan, Waziri Mkuu wa Sudan Abdullah Hamduk, Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit, Rais wa Somalia Muhammed Abdullah Fermacu, Rais wa Djibouti Ismail Omar Guelleh, Rais wa Chad Idris Debi, pamoja na wawakilishi kutoka Qatar, Falme za Kiarabu, Misri, Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa (UN).

Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu pamoja na nchi za Qatar, Misri, Jordan, Oman na Bahrain zilionyesha kuridhishwa na mkataba huo wa amani uliotiwa saini kati ya serikali ya Sudan na makundi ya waasi.

Mchakato wa makubaliano ya amani ulioanza tangu tarehe 14 Oktoba 2019 mjini Juba kati ya serikali ya Sudan na chama cha mapinduzi, yanajumuisha masuala ya kiusalama, umiliki wa ardhi, kurejeshwa kwa wakimbizi, haki za waathirika, fidia, kuunga mkono wahamaji na wachungaji wa mifuo, kugawana mali, mamlaka pamoja na hifadhi kwa waathirika wa mzozo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *