Serikali ya Afghanistan yawaachia wafungwa zaidi wa Taliban na kutoa nafasi ya mazungumzo ya amani, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on September 4, 2020 at 1:00 pm

September 4, 2020

Serikali ya Afghanistan imesema imewaachia wafungwa 400 wa Taliban chini ya makubaliano na wanamgambo hao. Maafisa wawili wa Taliban wamethibitisha kuachiwa kwa wafungwa hao ingawa wale ambao wanapingwa na Ufaransa na Australia bado wanazuiliwa na serikali. Ufaransa na Australia zinapinga kuachiwa kwa wafungwa hao kutokana na kuhusishwa kwao na mauaji ya wanajeshi na raia raia wa nchi hizo mbili nchini Afghanistan. Afghanistan inasema sasa inatarajia mazungumzo ya amani yaanze hivi karibuni. Pande hizo mbili zinazozozana zimekaribia kufanya mazungumzo ya moja kwa moja huko Qatar wiki hii, na kutilia kikomo hatua tata ya mwezi mzima ya kubadilishana wafungwa. Serikali ya Afghanistan tayari imeshatuma kikosi chake mjini Doha ambako afisi ya kisiasa ya Taliban ipo na mazungumzo yanatarajiwa kuanza hivi karibuni.,

Serikali ya Afghanistan imesema imewaachia wafungwa 400 wa Taliban chini ya makubaliano na wanamgambo hao. 

Maafisa wawili wa Taliban wamethibitisha kuachiwa kwa wafungwa hao ingawa wale ambao wanapingwa na Ufaransa na Australia bado wanazuiliwa na serikali. 

Ufaransa na Australia zinapinga kuachiwa kwa wafungwa hao kutokana na kuhusishwa kwao na mauaji ya wanajeshi na raia raia wa nchi hizo mbili nchini Afghanistan. 

Afghanistan inasema sasa inatarajia mazungumzo ya amani yaanze hivi karibuni. Pande hizo mbili zinazozozana zimekaribia kufanya mazungumzo ya moja kwa moja huko Qatar wiki hii, na kutilia kikomo hatua tata ya mwezi mzima ya kubadilishana wafungwa. 

Serikali ya Afghanistan tayari imeshatuma kikosi chake mjini Doha ambako afisi ya kisiasa ya Taliban ipo na mazungumzo yanatarajiwa kuanza hivi karibuni.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *