Serikali mbioni kujenga reli wilayani Ludewa,kurahisisha usafirishaji wa Chuma, on September 19, 2020 at 7:00 am

September 19, 2020

Na Amiri Kilagalila,NjombeSerikali inatarajia kuanza ujenzi wa reli kutoka Mtwara mpaka Mbambabay,huku matawi yakielekezwa Mchuchuma na Liganga wilayani Ludewa yanakopatinaka madini ya makaa yam awe na Chuma ili kurahisisha zaidi usafirishaji wa madini hayo.Hayo yamebainishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni mgombea mwenza wa Kiti cha Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) alipokuwa wilayani Ludewa kwa ajili ya kampeni za Chama hicho.“Katika kuupa nguvu mradi (Liganga na Mchuchuma) Serikali tunakwenda kujenga Reli kutoka Mtwara mpaka Mbambabay,Lakini matawi ya Reli yatakwenda Mchuchuma na Liganga,lengo ni kurahisisha usafirishaji wa Chuma na Liganga” alisema Samia Suluhu Hassan MgombeaVile vile Samia amesema mradi wa Liganga na Mchuchuma umechelewa kuanza kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo urekebishwaji wa mikataba kabla ya mradi huo haujaanza“Mchuchuma na Liganga ni mradi ambao umekaa muda mrefu haujaanza lakini ni imani yetu kwamba miaka mitano inayokuja mradi utaanza na katika kuendeleza mradi ule,tutaufanyia kazi kwa pamoja baina ya serikali na sekta binafsi.”alisema Samia Suluhu HassanKatika hatua nyingine kuhusu fidia kwa wananchi wanaopakana na miradi amesema “Tulikuwa na mazungumzo ya muda mrefu na muwekezaji,tumeelewana sasa mambo yako vizuri na kwa upande wa fidia,mkataba wa mradi unata fidia ilipwe na muwekezaji,lakini kuna ujanja umefanywa kuonyesha fidia ilipwe na serikali sasa hapo tunaendelea na mazungumzo.” Samia Suluhu HassanAwali kabla ya ufafanuzi wa mradi huo ambao umekuwa ukizungumzwa na kutegemewa na wakazi wa wilaya ya Ludewa,Mgombea wa Ubunge wa Jimbo hilo Wakili Joseph Kamonga aliposimama mbele ya wananchi kwa ajili ya kuomba kura,alieleza miradi mingi inayofanywa na serikali katika wilaya hiyo huku akigusia mradi huo wa Liganga.“Upo mradi mkubwa wa makaa ya mawe,Mchuchuma na Liganga ulifanyika uthamini kwa maana ya kulipa fidia lakini kwa bahati mbaya wananchi bado hawajalipwa fidia toka 2015,lakini wananchi wanasema bado wanaimani ya kulipwa fidia zao kwa kuwa wanajua uzalendo wa Rais wetu” alisema Joseph KamongHata hivyo ameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kutumia maji ya ziwa Nyasa ili kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji. “Tunaishukuru Serikali kwa miradi ya maji,lakini kama ambavyo imewezekana kutumia maji ya ziwa Victoria kutatua changamoto za maji.Serikali iangalie uwezekano wa kutumia maji ya ziwa Nyasa ili kutatua kero za wananchi kwenye tarafa ya Masasi” alisema Joseph KamongaBaadhi ya wananchi wa Ludewa waliohudhulia katika mkutano huo akiwemo Patrick Luoga na Menas Mbuligwe wanasema wanaimani na serikali yao hivyo shauku yao na kuona mradi wa Mchuchuma na Liganga unaanza ili kuinua uchumi wa Ludewa.,

Na Amiri Kilagalila,Njombe

Serikali inatarajia kuanza ujenzi wa reli kutoka Mtwara mpaka Mbambabay,huku matawi yakielekezwa Mchuchuma na Liganga wilayani Ludewa yanakopatinaka madini ya makaa yam awe na Chuma ili kurahisisha zaidi usafirishaji wa madini hayo.

Hayo yamebainishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni mgombea mwenza wa Kiti cha Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) alipokuwa wilayani Ludewa kwa ajili ya kampeni za Chama hicho.

“Katika kuupa nguvu mradi (Liganga na Mchuchuma) Serikali tunakwenda kujenga Reli kutoka Mtwara mpaka Mbambabay,Lakini matawi ya Reli yatakwenda Mchuchuma na Liganga,lengo ni kurahisisha usafirishaji wa Chuma na Liganga” alisema Samia Suluhu Hassan Mgombea

Vile vile Samia amesema mradi wa Liganga na Mchuchuma umechelewa kuanza kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo urekebishwaji wa mikataba kabla ya mradi huo haujaanza

“Mchuchuma na Liganga ni mradi ambao umekaa muda mrefu haujaanza lakini ni imani yetu kwamba miaka mitano inayokuja mradi utaanza na katika kuendeleza mradi ule,tutaufanyia kazi kwa pamoja baina ya serikali na sekta binafsi.”alisema Samia Suluhu Hassan

Katika hatua nyingine kuhusu fidia kwa wananchi wanaopakana na miradi amesema “Tulikuwa na mazungumzo ya muda mrefu na muwekezaji,tumeelewana sasa mambo yako vizuri na kwa upande wa fidia,mkataba wa mradi unata fidia ilipwe na muwekezaji,lakini kuna ujanja umefanywa kuonyesha fidia ilipwe na serikali sasa hapo tunaendelea na mazungumzo.” Samia Suluhu Hassan

Awali kabla ya ufafanuzi wa mradi huo ambao umekuwa ukizungumzwa na kutegemewa na wakazi wa wilaya ya Ludewa,Mgombea wa Ubunge wa Jimbo hilo Wakili Joseph Kamonga aliposimama mbele ya wananchi kwa ajili ya kuomba kura,alieleza miradi mingi inayofanywa na serikali katika wilaya hiyo huku akigusia mradi huo wa Liganga.

“Upo mradi mkubwa wa makaa ya mawe,Mchuchuma na Liganga ulifanyika uthamini kwa maana ya kulipa fidia lakini kwa bahati mbaya wananchi bado hawajalipwa fidia toka 2015,lakini wananchi wanasema bado wanaimani ya kulipwa fidia zao kwa kuwa wanajua uzalendo wa Rais wetu” alisema Joseph Kamong

Hata hivyo ameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kutumia maji ya ziwa Nyasa ili kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji.

 “Tunaishukuru Serikali kwa miradi ya maji,lakini kama ambavyo imewezekana kutumia maji ya ziwa Victoria kutatua changamoto za maji.Serikali iangalie uwezekano wa kutumia maji ya ziwa Nyasa ili kutatua kero za wananchi kwenye tarafa ya Masasi” alisema Joseph Kamonga

Baadhi ya wananchi wa Ludewa waliohudhulia katika mkutano huo akiwemo Patrick Luoga na Menas Mbuligwe wanasema wanaimani na serikali yao hivyo shauku yao na kuona mradi wa Mchuchuma na Liganga unaanza ili kuinua uchumi wa Ludewa.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *