Septemba 11, Ni Mungu Pekee ndiye Anajua Kilichotokea!

September 11, 2020

HABARI nyingi kupita kiasi, husumbua ubongo wa mwanadamu.Lakini kwa kutazama mambo kwa uangalifu, ni bora zaidi kuwa na habari nyingi kuliko kutokuwa na habari zozote. Au ni bora kuwa na habari nyingi kuliko kutokuwa na habari kabisa. Lakini inakuwa mbaya zaidi tunapokuwa na habari tunazofi kiri kwamba zinatosha, kumbe ni habari za uongo au kudanganywa.Leo ni kumbukumbu ya tukio kubwa na la kutisha la SEPTEMBA 11. Gazeti la IJUMAA linakuchambulia kile kilichojiri siku hiyo yapata miaka 19 iliyopita. Ni tukio lililoionjesha Nchi ya Marekani kiyama!NI TUKIO LA KUTATANISHA KULIKO LINGINE LOLOTE.Nani aliyefanya mashambulizi dhidi ya Marekani Septemba 11, 2001? Yalikuwa na lengo gani? Kwa nini yalifanyika Septemba 11 badala ya siku nyingine yoyote? Itoshe kusema kuwa, tukio hili lina maswali mengi kuliko majibu. Watu huamini kile wanachoona, saikolojia halisi haikubaliani na hekima hiyo. Badala yake, saikolojia hiyo inasema kwamba, watu huona kile wanachoamini na wala si kwamba huamini kile wanachoona!Tukio la Septemba 11, 2001 (miaka 19 iliyopita), limejengewa taswira nyingi, kubwa ni tukio la kutengenezwa.Kwenye Kipindi cha The Story Book cha Profesa Jamal anasema, wapo wanaodai kuwa Rais wa Marekani wa wakati huo, George W. Bush na watu wake, ndiyo waliofanya tukio.Lakini wengi wanaamini aliyefanya ni Osama Bin Laden na Kundi la Alcaeda. Wengine wanaamini kuwa ni Waisraeli.Namba 11 ni ishara inayotumiwa kwa malengo fulani. Kisha kuna namba 911, ambayo nayo ina namba 11. Hii, kwa wale wanaofuata mambo ya unajimu, wanaweza kudhani kuwa ninachoandika hapa ni njozi ya mchana.Ukitazama majengo yaliyoangushwa Marekani jinsi yalivyokuwa yamesimama, utaona namba 11 kwa sababu ni minara miwili iliyokaa sambamba, na ndege ya kwanza kugonga majengo hayo Septemba 11, ni Flight 11.Kutokea mara kwa mara kwa namba 11 katika tukio la Septemba 11, ni jambo la ajabu kwa wengi.Makao Makuu ya Jeshi la Marekani (Pentagon), ndiyo yaliyozungukwa zaidi na muujiza huu wa namba 11, hasa Septemba 11 au tuseme 911. Ndege inayodaiwa kugonga Pentagon, ni Flight 77.Ukiigawa 77 kwa 7 utapata 11 na katika hiyo 7-1-1=5. Namba tano ndiyo namba halisi ya The Pentagon. Tafsiri ya Pentagon, ni kitu chenye pembe 5.Jengo la Pentagon, lilianza kujengwa kutokana na maombi ya Brigedia Jenerali Brehon. Hatimaye jiwe la msingi likawekwa Septemba 11, 1941.Jumanne ya Mei 22, 1962, (22 inahusiana moja kwa moja na namba 11) ndege ya Shirika la Continental, Flight 11, 707, ilikuwa ndege ya kwanza kuhujumiwa wakati bomu lilipolipuka na kuua watu wote 45.Septemba 11, 1998, mwanasheria Kenneth Starr, alituma taarifa iliyojulikana kama The Starr Report, kwenda Bunge la Marekani, ikimshutumu Rais Bill Clinton kwa makosa 11 yaliyokuwa na uzito wa kutosha, kumuondosha madarakani. Mwaka 1967 nchini Marekani, ilipendekezwa kubuniwa namba moja, ambayo ingekuwa ya dharura kwa Taifa lote la nchi hiyo. Kampuni ya Simu ya Marekani (AT&T), mwaka 1968, ilitangaza kuanzisha namba 911 au tisa moja moja au tisa-kumi-na-moja (nine-eleven). Kuanzia wakati huo, Septemba 11 ilikuwa ikitazamwa kama siku ya dharura katika Taifa hilo. Mambo hayo yalibadilika mara baada ya tukio la Septemba 11. Canada nayo, mwaka 1980, ilianza kutumia namba hiyo ya dharura, 911. Je, ni jambo la bahati mbaya kwamba namba 11 na 9, pamoja na zile nyingine kama 22, 33, 44, 55, 66 na 77 zinajirudiarudia? Kama unadhani huu ni unajimu, tafakari kwa umakini.Tarehe ya mashambulizi ya Marekani; 9/11 – 9 + 1 + 1 = 11. Septemba 11 ni siku ya 254 ya mwaka; 2 + 5 + 4 = 11.Baada ya Septemba 11, kuna siku 111 zilizobaki hadi kumalizika kwa mwaka. 119 ni namba ya mwito wa simu wa Iraq na Iran kama Tanzania ilivyo na 255. Na 1 + 1 + 9 = 11.Majengo ya WTC, yakiwa yamesimama sambamba, huonekana kama namba 11. Ndege ya kwanza kugonga jengo la kwanza ilikuwa ni Flight 11.Lakini kuna mengi zaidi ya hayo. Jimbo la New York, ni la 11 kuingizwa Marekani. Ukisoma vyema herufi za neno New York City, utagundua kuwa ziko 11. Neno Afghanistan ambayo inahusishwa na Septemba 11, ina herufi 11. Neno The Pentagon, nalo lina herufi 11. Jina la Ramzi Yousef anayedaiwa kuendesha mashambulizi ya WTC mwaka 1993, lina herufi 11. Flight 11, ikiwa na abiria 92 ndani yake, hesabu yake ni (92) 9 + 2 = 11. Ndege ya Flight 77, ikiwa na abiria 65 ndani yake, ukipanga tarakimu zake, utapata 6 + 5 = 11.Tarehe ya mashambulizi; 11/9; 11 – 9 = 2. September 11 = 1 + 1 = 2. Septemba 11 ni siku ya 254 ya mwaka; 2 + 5 + 4 = 11 na 11 ni sawa na 1 + 1 = 2. Majengo ya World Trade Center, yalikuwa na minara miwili iliyogongwa na ndege mbili.Namba 11 imehusishwa na nguvu za siri tangu zamani za kale. Aina zote za utafi ti wa namba zinatoa umuhimu kwa namba 11 na zile zinazohusiana nayo kama 22, 33, 44, 55, 66, 77, 88 na 99.Namba 11 hufi kiriwa kuwa kuu zaidi ya zote. Vita Kuu ya Kwanza ilimalizika saa ya 11, siku ya 11 katika mwezi wa 11, mwaka 1918. Kwa baadhi ya Wamarekani wanajua umuhimu wa namba 11. Kuna mengi yaliyojifi cha kuliko yale tunayoyajua. Tukio la Septemba 11 lina utata ambao ni vigumu kuutatua. Vyombo vya habari vimeandika tu yale ambayo watawala walitaka yaandikwe. Ukweli wote wa kilichotokea, ni Mungu pekee anayejua!,

HABARI nyingi kupita kiasi, husumbua ubongo wa mwanadamu.Lakini kwa kutazama mambo kwa uangalifu, ni bora zaidi kuwa na habari nyingi kuliko kutokuwa na habari zozote. Au ni bora kuwa na habari nyingi kuliko kutokuwa na habari kabisa.

 

Lakini inakuwa mbaya zaidi tunapokuwa na habari tunazofi kiri kwamba zinatosha, kumbe ni habari za uongo au kudanganywa.Leo ni kumbukumbu ya tukio kubwa na la kutisha la SEPTEMBA 11.

 

Gazeti la IJUMAA linakuchambulia kile kilichojiri siku hiyo yapata miaka 19 iliyopita. Ni tukio lililoionjesha Nchi ya Marekani kiyama!

NI TUKIO LA KUTATANISHA KULIKO LINGINE LOLOTE.

Nani aliyefanya mashambulizi dhidi ya Marekani Septemba 11, 2001? Yalikuwa na lengo gani? Kwa nini yalifanyika Septemba 11 badala ya siku nyingine yoyote? Itoshe kusema kuwa, tukio hili lina maswali mengi kuliko majibu.

 

Watu huamini kile wanachoona, saikolojia halisi haikubaliani na hekima hiyo. Badala yake, saikolojia hiyo inasema kwamba, watu huona kile wanachoamini na wala si kwamba huamini kile wanachoona!Tukio la Septemba 11, 2001 (miaka 19 iliyopita), limejengewa taswira nyingi, kubwa ni tukio la kutengenezwa.

Kwenye Kipindi cha The Story Book cha Profesa Jamal anasema, wapo wanaodai kuwa Rais wa Marekani wa wakati huo, George W. Bush na watu wake, ndiyo waliofanya tukio.Lakini wengi wanaamini aliyefanya ni Osama Bin Laden na Kundi la Alcaeda. Wengine wanaamini kuwa ni Waisraeli.Namba 11 ni ishara inayotumiwa kwa malengo fulani. Kisha kuna namba 911, ambayo nayo ina namba 11.

 

Hii, kwa wale wanaofuata mambo ya unajimu, wanaweza kudhani kuwa ninachoandika hapa ni njozi ya mchana.Ukitazama majengo yaliyoangushwa Marekani jinsi yalivyokuwa yamesimama, utaona namba 11 kwa sababu ni minara miwili iliyokaa sambamba, na ndege ya kwanza kugonga majengo hayo Septemba 11, ni Flight 11.Kutokea mara kwa mara kwa namba 11 katika tukio la Septemba 11, ni jambo la ajabu kwa wengi.Makao Makuu ya Jeshi la Marekani (Pentagon), ndiyo yaliyozungukwa zaidi na muujiza huu wa namba 11, hasa Septemba 11 au tuseme 911. Ndege inayodaiwa kugonga Pentagon, ni Flight 77.

Ukiigawa 77 kwa 7 utapata 11 na katika hiyo 7-1-1=5. Namba tano ndiyo namba halisi ya The Pentagon. Tafsiri ya Pentagon, ni kitu chenye pembe 5.Jengo la Pentagon, lilianza kujengwa kutokana na maombi ya Brigedia Jenerali Brehon.

 

Hatimaye jiwe la msingi likawekwa Septemba 11, 1941.Jumanne ya Mei 22, 1962, (22 inahusiana moja kwa moja na namba 11) ndege ya Shirika la Continental, Flight 11, 707, ilikuwa ndege ya kwanza kuhujumiwa wakati bomu lilipolipuka na kuua watu wote 45.Septemba 11, 1998, mwanasheria Kenneth Starr, alituma taarifa iliyojulikana kama The Starr Report, kwenda Bunge la Marekani, ikimshutumu Rais Bill Clinton kwa makosa 11 yaliyokuwa na uzito wa kutosha, kumuondosha madarakani.

 

Mwaka 1967 nchini Marekani, ilipendekezwa kubuniwa namba moja, ambayo ingekuwa ya dharura kwa Taifa lote la nchi hiyo. Kampuni ya Simu ya Marekani (AT&T), mwaka 1968, ilitangaza kuanzisha namba 911 au tisa moja moja au tisa-kumi-na-moja (nine-eleven).

 

Kuanzia wakati huo, Septemba 11 ilikuwa ikitazamwa kama siku ya dharura katika Taifa hilo. Mambo hayo yalibadilika mara baada ya tukio la Septemba 11. Canada nayo, mwaka 1980, ilianza kutumia namba hiyo ya dharura, 911.

 

Je, ni jambo la bahati mbaya kwamba namba 11 na 9, pamoja na zile nyingine kama 22, 33, 44, 55, 66 na 77 zinajirudiarudia? Kama unadhani huu ni unajimu, tafakari kwa umakini.Tarehe ya mashambulizi ya Marekani; 9/11 – 9 + 1 + 1 = 11. Septemba 11 ni siku ya 254 ya mwaka; 2 + 5 + 4 = 11.

Baada ya Septemba 11, kuna siku 111 zilizobaki hadi kumalizika kwa mwaka.

 

119 ni namba ya mwito wa simu wa Iraq na Iran kama Tanzania ilivyo na 255. Na 1 + 1 + 9 = 11.Majengo ya WTC, yakiwa yamesimama sambamba, huonekana kama namba 11. Ndege ya kwanza kugonga jengo la kwanza ilikuwa ni Flight 11.Lakini kuna mengi zaidi ya hayo. Jimbo la New York, ni la 11 kuingizwa Marekani. Ukisoma vyema herufi za neno New York City, utagundua kuwa ziko 11.

 

Neno Afghanistan ambayo inahusishwa na Septemba 11, ina herufi 11. Neno The Pentagon, nalo lina herufi 11. Jina la Ramzi Yousef anayedaiwa kuendesha mashambulizi ya WTC mwaka 1993, lina herufi 11.

 

Flight 11, ikiwa na abiria 92 ndani yake, hesabu yake ni (92) 9 + 2 = 11. Ndege ya Flight 77, ikiwa na abiria 65 ndani yake, ukipanga tarakimu zake, utapata 6 + 5 = 11.Tarehe ya mashambulizi; 11/9; 11 – 9 = 2. September 11 = 1 + 1 = 2. Septemba 11 ni siku ya 254 ya mwaka; 2 + 5 + 4 = 11 na 11 ni sawa na 1 + 1 = 2.

 

Majengo ya World Trade Center, yalikuwa na minara miwili iliyogongwa na ndege mbili.Namba 11 imehusishwa na nguvu za siri tangu zamani za kale.

 

Aina zote za utafi ti wa namba zinatoa umuhimu kwa namba 11 na zile zinazohusiana nayo kama 22, 33, 44, 55, 66, 77, 88 na 99.Namba 11 hufi kiriwa kuwa kuu zaidi ya zote. Vita Kuu ya Kwanza ilimalizika saa ya 11, siku ya 11 katika mwezi wa 11, mwaka 1918. Kwa baadhi ya Wamarekani wanajua umuhimu wa namba 11.

 

Kuna mengi yaliyojifi cha kuliko yale tunayoyajua. Tukio la Septemba 11 lina utata ambao ni vigumu kuutatua. Vyombo vya habari vimeandika tu yale ambayo watawala walitaka yaandikwe. Ukweli wote wa kilichotokea, ni Mungu pekee anayejua!

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *