Semenya Apoteza Rufaa ya Kizuizi cha Viwango vya Homoni

September 9, 2020

Mwanariadha wa Afrika Kusini Caster Semenya amepoteza rufaa dhidi ya kizuizi cha viwango vya homoni ya kiume kwa wanariadha wa kike aliyowasilisha mbele ya mahakama ya juu zaidi ya riadha nchini Uswizi.Semenya haruhusiwi kushiriki mbio za kati ya mita 400 na maili moja bila kutumia dawa za kupunguza viwango vya homoni ya kiume, uamuzi uliofikiwa 2019 na shirikisho la riadha duniani.”Nimesikitika sana,” alisema mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 29.Shirikisho la riadha liliweka sheria kwamba wanariadha walio na tofauti za ukuaji wa kijinsia lazima watumie dawa maalum ili kushindana katika mbio za mita 400 hadi maili moja la sivyo wakimbie mbio ndefu zaidi.,

Mwanariadha wa Afrika Kusini Caster Semenya amepoteza rufaa dhidi ya kizuizi cha viwango vya homoni ya kiume kwa wanariadha wa kike aliyowasilisha mbele ya mahakama ya juu zaidi ya riadha nchini Uswizi.

Semenya haruhusiwi kushiriki mbio za kati ya mita 400 na maili moja bila kutumia dawa za kupunguza viwango vya homoni ya kiume, uamuzi uliofikiwa 2019 na shirikisho la riadha duniani.

“Nimesikitika sana,” alisema mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 29.

Shirikisho la riadha liliweka sheria kwamba wanariadha walio na tofauti za ukuaji wa kijinsia lazima watumie dawa maalum ili kushindana katika mbio za mita 400 hadi maili moja la sivyo wakimbie mbio ndefu zaidi.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *