Sayari ya ‘Mars’ sasa hivi ni ‘kubwa na inang’aa zaidi’

October 12, 2020

Dakika 20 zilizopita

Mars pictured by Damian Peach on 30 September

Sayari ya Mars sasa hivi ni kubwa na inayong’aa zaidi wakati ambapo zote yaani pamoja na Dunia ziko upande mmoja na Jua.

Kila miezi 26, dunia na mihiri yaani mars hukutana upande mmoja, na kusongeleana kwa karibu kabla ya kila moja kushika njia yake kwenye mzunguko wake.

Jumanne usiku ni wakati wa kuona muonekano huo wa kuvutia ambao wanaanga huuita “opposition” kwa kiingereza.

Zote tatu zitakuwa kwenye mstari mmoja yaani Dunia, Mahiri na Jua ifikapo saa tano na dakika 20 usiku.

“Lakini huna haja ya kusubiri hadi usiku wa manane; kwa sababu hata kipindi hiki, saa tatu au nne usiku, unaweza kuona muonekano huo kusini mashariki,” amesema mpiga picha wa anga za mbali, Damian Peach.

“Huwezi kukosa kutazama tukio hili la kipeke, ni nyota inayong’aa zaidi kwenye anga,” amezungumza na BBC.

Umbali wa kilomita 62,069,570 au maili 38,568,243. Huo ni umbali mdogo zaidi hadi mwaka 2035.

Tukio la mwisho la namna hii, mwaka 2018, Sayari ya Dunia na Mars zilikuwa umbali wa kilomita 58 pekee lakini kinachofanya tukio la sasa hivi kuwa la kipekee zaidi kwa wapiga picha wa anga za mbali upande wa kizio cha Kaskazini ni mwinuko wa nyota ya mihiri kwenye anga.

Iko juu na hiyo inamaanisha hakuna haja ya kutumia darubini kuangalia sana kwenye anga hewa lenye kutikisika ambayo huaribu picha.

Wapiga picha waliobobea kama Damian hutumia mbinu maalum kupata picha nzuri. Huchukua muda kupima umbali wa picha na kutumia programu maalum kuunganisha pamoja muonekano wenye kuvutia zaidi.

Picha ya Damian juu ya ukurasa huu inaonesha “Mgawanyiko wa Mars” – inayoonesha utofauti uliopo kati ya nyanda za chini zilizonyooka upande wa Kaskazini maeneo yenye mabonde upande wa kizio wa Kusini.

Kinachooneka vizuri zaidi pia ni kilele cha barafu cha kaboni kwenye ncha ya kusini.

Picha hiyo ilichukuliwa kwa kutumia darabuni ya Celestron ya nchi 14.

“Hicho ni kifaa cha ghali na sio rahisi kukipata,” amesema Damian. “Lakini hata darubini ambayo ukubwa wake ni nusu ya hiyo, itaonesha vilivyomo vyote kwenye sayari ya Mihiri tena kwa urahisi.

Na ikiwa utakuwa na darubini nzuri, bila shaka utaweza kuona sayari wala sio nyota tu.”

Artwork: Hope

Maelezo ya picha,

Mchoro wa Hope

Presentational white space

Vyombo vya anga vinavyorushwa kutoka kwenye dunia kwenda kwenye sayari ya Mihiri hurushwa eneo hilo.

Bila shaka umbali chombo hicho kinastahili kukutana ni mfupi na muda a nguvu inayohitajika kwa safari hiyo kufanikiwa ni kidogo.

Safari zote za kwenda kwenye sayari ya mihiri ambazo vyombo vyake viilirushwa Julai sasa hivi viko njiani:

Chombo cha Hope cha Falme za Kiarabu; Chombo cha Tianwen; na kile cha Perseverance cha Marekani.

Ulaya na Urusi zilikuwa na matumaini ya kutuma vyombo yao vya anga pia lakini wakashindwa kufikia tarehe iliyokuwa imetengwa na sasa hivi watahitajika kusubiri hadi baadae mwaka 2022.

Hiyo ndio adhabu yake wakati ambapo dunia na sayari ya mihiri zinakutana kila kwa miezi 26 pekee.

Vyombo vya ‘Hope, Tianwen na Perseverance’ vyote vinatarajiwa kuwasili kwenye Sayari.

Mwaka 2003, Sayari ya Mars ilifika karibu sana na Dunia katika kipindi cha karibu miaka 69,000 – umbali wa kilomita milioni 56 pekee.

Umbali kati ya dunia na mihiri unaweza kuwa zaidi ya kilomita 100 kama ilivyokuwa mwaka 2012.

Mabadiliko hayo yanatokana na umbo la mviringo la mzunguko wa Mars na Dunia.

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *