SAKATA la Shujaa wa Hotel Rwanda Kutekwa.. KAGEME Afunguka

September 7, 2020

Rais wa Rwanda Paul Kagame amekana jana kuwa serikali yake ilimteka kutoka nje ya nchi hiyo Paul Rusesabagina, ambaye madai yaliyopo ya ushujaa wake yamechangia utengenezaji wa filamu ya Hollywood lakini amekamatwa hivi sasa kwa madai ya ugaidi pamoja na madai mengine. Katika mkutano na waandishi habari uliofanyika kwa njia ya vidio mjini Kigali, Kagame hakusema ni vipi hasa Rusesabagina alitiwa kizuwizini lakini alieleza kwamba alidanganywa na kusafiri kwenda Rwanda kabla ya kukamatwa. Kagame alisema hakukuwa na tukio la kutekwa. Na hakuna kitu kilichofanyika kinyume na sheria katika mchakato wa kumpata.Aliingia hapa Kagame alisema , kwa misingi ya kile alichoamini na kutaka kukifanya, na alijikuta hapa, hicho ndicho kilichotokea.Serikali ya Rwanda ilitangaza kukamatwa kwa Rusesabagina Agosti 31 akioneshwa mbele ya waandishi habari akiwa amefungwa pingu.,

Rais wa Rwanda Paul Kagame amekana jana kuwa serikali yake ilimteka kutoka nje ya nchi hiyo Paul Rusesabagina, ambaye madai yaliyopo ya ushujaa wake yamechangia utengenezaji wa filamu ya Hollywood lakini amekamatwa hivi sasa kwa madai ya ugaidi pamoja na madai mengine.
 Katika mkutano na waandishi habari uliofanyika kwa njia ya vidio mjini Kigali, Kagame hakusema ni vipi hasa Rusesabagina alitiwa kizuwizini lakini alieleza kwamba alidanganywa na kusafiri kwenda Rwanda kabla ya kukamatwa.

 Kagame alisema hakukuwa na tukio la kutekwa. Na hakuna kitu kilichofanyika kinyume na sheria katika mchakato wa kumpata.

Aliingia hapa Kagame alisema , kwa misingi ya kile alichoamini na kutaka kukifanya, na alijikuta hapa, hicho ndicho kilichotokea.

Serikali ya Rwanda ilitangaza kukamatwa kwa Rusesabagina Agosti 31 akioneshwa mbele ya waandishi habari akiwa amefungwa pingu.,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *