Sagini aguswa na wagonjwa wanaofia njiani,

October 8, 2020

Mbunge mteule wa Jimbo la Butiama kupitia tiketi Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mara Jumanne Sagini amewaahidi wananchi wa Kijiji cha Nyakiswa Kata ya Kyanyari kuwakamilishia jengo la kituo cha afya ili kupugunza vifo vya mama na mtoto pamoja na wagonjwa wa wanaopatwa na mauti wakitafuta huduma za matibabu kwa muda kwa umbali mrefu.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni amesema kuwa tangu uhuru wananchi wa kijiji hicho walikuwa wanaifata huduma hiyo Kata Madaraka Kiabakari takribani kilomita 8 huku miundombinu ikiwa hafifu jambo lililopelekea baadhi yao kushindwa kufika kupata matibabu na kina mama wajawazito kujifungulia njiani.

“Mimi ni mkombozi wenu nitahakikisha mnapata huduma bora ya afya bila kutembea mwendo mrefu, nawaomba wananchi kutunza mradi huu kila mmoja awe mlinzi wa mwenziye katika hasa viletwapo vifaa vya kukamilishia ujenzi vinavyotarajia kuletwa hivi karibuni,” amesema Sagini.

Awali mbunge huyo alipokea maswali juu ya ukamilishaji kituo cha afya kilichokaa muda mrefu ambapo ujenzi wa boma ulijengwa kwa nguvu za wananchi wakiwa wamechangia zaidi ya shilingi milioni 80 bila mafanikio.

Aidha Mbunge huyo ameeleza kuwa fedha za ukamilikishaji wa kituo hicho zimeshatengwa na zitaanza na zitapelekwa kufanya kazi iliyokusudiwa na kuwaomba wananchi kumpigia kura za ndio Mgombea wa Urais wa Awamu ya Tano Dkt John Magufuli kwa mandeleo yanaonekana.

 

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *