Safari za ndege zarejea Afrika Kusini,

October 2, 2020

 

Ndege za mashirika kadhaa ya kikanda na kimataifa zimetua kwa mara ya kwanza jana nchini Afrika Kusini baada ya taifa hilo kufungua mipaka yake tangu ilipofungwa miezi sita iliyopita kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona. 

 Shirika la ndege la Ujerumani Lufthansa limekuwa la kwanza kutoka barani Ulaya kurejesha huduma nchini humo kwa ndege yake iliyotokea mjini Frankfurt kutua katika Uwanja wa ndege wa Oliver Tambo mjini Johannesburg. 

Ndege kutoka mataifa ya Kenya, Zambia na taifa jirani la Zimbabwe pia zilitua jana mjini Johannesburg. Afrika Kusini, moja ya mataifa yenye uchumi mkubwa barani Afrika ilifunga mipaka yake wakati ilipotangaza vizuizi vikali vya kusafiri mnamo Machi 27 katika juhudi za kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa COVID-19. 

Nchi hiyo imeathiriwa vibaya na maradhi hayo yaliyosababisha vifo vya watu 16,734 na kuambukiza jumla ya watu 674,339.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *