Rwanda yapunguza muda wa amri ya kutotoka nje usiku,

October 13, 2020

Wanaokiuka miongozo ya kukabiliana na corona Rwanda hulazimishwa kuketi hadi siku inayofuataImage caption: Wanaokiuka miongozo ya kukabiliana na corona Rwanda hulazimishwa kuketi hadi siku inayofuata

Baraza la mawziri nchini Rwanda limepunguza muda wa amri ya kutotembea nje wakati wa usiku kwa saa mbili huku idadi ya watu wapya walinaopata maambukizi ikipungua.

Amri ya kutotembea nje usiku sasa itaanza kutekelezwa kuanzia saa nne usiku hadi saa kumi alfajiri kwa saa za Rwanda.

Sasa mabasi ya abiria ya umma yatajaza vitri vyote vya abiria huku idadi ya abiria wanaosimama wakiruhusiwa kuwa nusu ya wale waliokuwa wakiruhusiwa kusimama ndani ya basi.

Watu wanaohudhuria mikutano hawatahitajika tena kudhihirisha kuwa hawana Covid-19, lakini waandalizi watatakiwa kuheshimu miongozo ya kukaa mbali kwakwa kuwa na 50% ya mahudhurio ya washiriki.

Baraza la mawaziri limesema kuwa adhabu ya kutovaa barakoa na kukiuka amri ya kutotoka nje itaendelea kutekelezwa.

Wale wanaopatikana bila kuvaa barakoa katika maeneo ya umma watatozwa faini ya$10. Kiwango hicho cha faini pia kitatozwa kwa wale wasioheshimu miongozo ya kukaa umbali wa mita 2 kati ya mtu na mtu na kupuuza amri ya kutotoka nje nyakatoi za usiku.

Baadhi ya watu wanaokiuka maagizo hayo hulala kwenye viwanja vya michezo au majengo ya shule ambako huketi hadi asubuhi ya siku inayofuata.

Hadi sasa Rwanda imethibitisha kuwa watu 4,905 walipatwa na maambukizi ya virusi vya corona

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *