Ruvu Shooting yaaidi kupata ubingwa leo katika mchezo wake na Dodoma jiji FC,

October 2, 2020

 

UONGOZI wa timu ya Ruvu Shooting umeweka wazi kuwa unajiamini katika uwezo wao na utapambana kupata matokeo chanya kwenye mechi yao dhidi ya Dodoma Jiji FC leo Oktoba 2.

Ruvu Shooting inakutana na Dodoma Jiji ambayo imecheza mechi nne mpaka sasa na kupoteza mechi moja mbele ya Polisi Tanzania 3-0, sare ya bila kufungana na Coastal Union na kushinda mechi mbili mbele ya JKT Tanzania 0-2 Dodoma, Dodoma 1-0 Mwadui.

 Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa Ruvu imejipanga kupata matokeo mazuri bila ya kujali kuwa wanacheza nyumbani ama ugenini, kwao hiyo halitakuwa kikwazo cha kuwafanya washindwe kupata pointi 3.

“Ruvu inauhakika kwa maandalizi yote tuliyofanya na uwezo tulionao tutafanikiwa kuwapatia mashabiki wetu matokeo chanya bila ya kujali kama tuko nyumbani au ugenini.

“Kwa mtu ambaye yuko kwenye maandalizi ya mpira na anajua kucheza mpira kamwe hawezi kushinda nyumbani peke yake, popote atashinda tu. Sasa niwaambie wadau wote wa Ruvu Shooting kuwa sisi tumejipanga vizuri, jambo linalotupa tiketi ya ushindi mkubwa dhidi ya Dodoma na kikosi chochote tutakachokumbana nacho. Popote tutashinda tu,” amesema Bwire.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *