Rouhani asema Marekani yakabiliwa na upinzani kwa kuiwekea vikwazo Iran, on September 20, 2020 at 5:00 pm

September 20, 2020

 Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema leo kwamba Marekani inakabiliwa na kushindwa katika hatua yake ya kuweka tena vikwazo vya Umoja wa Mataifa kwa nchi hiyo huku Marekani ikitangaza kuwa vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran vimedumishwa. Rouhani ameongeza kusema kwamba Marekani inakabiliwa na pingamizi kutoka kwa jumuiya ya kimataifa na kwamba haitakubali shinikizo hizo za Marekani. Muda mchache baada ya Marekani kutangaza kurejesha vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran, washirika wake muhimu duniani wamejitenga nayo, wakisema haina uhalali huo. Ufaransa, Uingereza na Ujerumani – ambazo kawaida ni washirika wa Marekani – zilitowa taarifa ya pamoja zikisema hatua hiyo ya Marekani haina nguvu yoyote ya kisheria. Kauli kama hiyo ilitolewa pia na Urusi, hasimu mkubwa wa Marekani. Taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Urusi imesema kuwa hatua na vitendo vilivyo kinyume na sheria vya Marekani kimsingi haviwezi kuwa na athari ya kisheria kwa nchi nyengine.,

 

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema leo kwamba Marekani inakabiliwa na kushindwa katika hatua yake ya kuweka tena vikwazo vya Umoja wa Mataifa kwa nchi hiyo huku Marekani ikitangaza kuwa vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran vimedumishwa. 

Rouhani ameongeza kusema kwamba Marekani inakabiliwa na pingamizi kutoka kwa jumuiya ya kimataifa na kwamba haitakubali shinikizo hizo za Marekani. Muda mchache baada ya Marekani kutangaza kurejesha vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran, washirika wake muhimu duniani wamejitenga nayo, wakisema haina uhalali huo. 

Ufaransa, Uingereza na Ujerumani – ambazo kawaida ni washirika wa Marekani – zilitowa taarifa ya pamoja zikisema hatua hiyo ya Marekani haina nguvu yoyote ya kisheria. Kauli kama hiyo ilitolewa pia na Urusi, hasimu mkubwa wa Marekani. Taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Urusi imesema kuwa hatua na vitendo vilivyo kinyume na sheria vya Marekani kimsingi haviwezi kuwa na athari ya kisheria kwa nchi nyengine.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *