Rose Ndauka na mumewe wapata mtoto,

October 8, 2020

 

Msanii wa filamu na tamthilia hapa nchini, mwanadada Rosse Ndauka na mumewe Haffiy wamebarikiwa kupata mtoto wao wa kwanza pamoja. Taarifa hiyo ya Rose kujifungua imethibitishwa na yeye mwenyewe kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Hii ni baada ya Jumatano hii Oktoba 7, kuposti picha akiwa na familia yake aliyoiambatanishia ujumbe wa kumshukuru M/Mungu, “Thanks God for another gift ❤️❤️❤️” – Rosa aliandika.

Sambamba na hilo, #Rose leo anasherehekea tarehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, akiwa tayari ametimiza umri wa miaka 31, kwa mujibu wa taarifa anatajwa kujifungua salama huku jinsia ya mtoto wake ikitajwa kuwa ni wakiume.

Huyu anakuwa mtoto wa pili kwa #Rose baada ya Naveen (wakike), aliyempata mwaka 2014.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *