Ronaldo asema viwanja vitupu ni kama sarakasi bila wachekeshaji

September 9, 2020

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ureno, alifunga bao lake la 100 na 101 kwa nchi yake katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sweden Jumanne (08.09.2020) katika ligi ya soka ya mataifa.

“Ni kama kwenda kwenye sarakasi bila mchekeshaji aliyevalia vazi la kuchekesha katika, kwenda kwenye bustani bila maua,” alisema Ronaldo na kuongeza, “Hatupendi kama wachezaji, lakini tayari nimezoea. Ninatafakari kabla ya mechi tayari nikijua kuwa uwanja utakuwa mtupu.”

Fußball Champions League I Juventus vs Olympique Lyonnais (Reuters/M. Pinca)

Cristiano Ronaldo uwanjani

Ronaldo alisema kuwa amekosa hata mashabiki wapinzani. “Inasikitisha,” alisema mshambuliaji huyo wa klabu ya Juventus ya Italia. “Ninapenda wakati ninapodhihakiwa katika mechi za ugenini, inanipa motisha. Lakini suala la afya linatakiwa kupewa kipaumbele na tunahitaji kuheshimu hilo. Lakini inasikitisha.”

Aidha Ronaldo alisema ana matumaini kuwa “ndani ya miezi michache”mashabiki wanaweza kurudi viwanjani kwa sababu wao ndio “furaha” ya mchezo wa soka.

Kwa magoli yake dhidi ya Sweden, Ronaldo amekuwa mchezaji wa pili tu wa kiume kufikia magoli 100 katika mpira wa miguu wa kimataifa. Anamfuatia tu mshambuliaji wa zamani wa Iran, Ali Daei, ambaye aliifungia timu yake ya taifa mabao 109.

Chanzo: AP

Source link

,Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ureno, alifunga bao lake la 100 na 101 kwa nchi yake katika ushindi wa mabao…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *