Ronald Koeman: Dhamira ya Messi Barcelona haimithiliki

October 5, 2020

Luuk de Jong ndiye aliyewafungia Sevilla katika dakika ya nane ila Philipe Coutinho alisawazisha baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Lionel Messi.

Kocha wake Ronald Koeman amesema Muargentina huyo amekuwa mfano kwa wachezaji wengine tangu alipoamua kusalia kuwa mchezaji wa Barca kwani kulikuwa na hofu kwamba hatojitolea kama awali kuichezea klabu hiyo baada ya uhamisho wake kuelekea Manchester City kuvunjika.

“Hakuna mjadala, kulingana na mimi amekuwa mchezaji bora duniani, nilikuwa na wazo hilo tangu kitambo na hata sasa ninapofanya kazi naye. Dhamira yake iko hapa kikamilifu na ni mfano kwa kila mmoja kwa jinsi nahodha anavyostahili kuwa,” alisema Koeman.

 

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *