Robert Lewandowski mchezaji bora wa Mwaka Ulaya,

October 2, 2020

Mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski ameshinda tuzo ya UEFA ya mchezaji bora wa mwaka barani Ulaya. 

Lewandowski mwenye miaka 32 aliwashinda wachezaji wenzake Manuel Neuer na Kevin De Bruyne kutoka Manchester City.

 Mshambuliaji huyo nyota alifunga mabao 55 katika michezo 47 ya mwaka 2019/20. Aidha Manuel Neuer ameshinda tuzo ya mlinda lango bora, beki bora ni Joshua Kimmich, na kocha bora ni Hansi Flick, wote watatu wanatokea timu ya Bayern Munich.

 Kwa upande wa wanawake, Pernille Harder mchezaji wa zamani wa Wolfsburg kutoka Denmark ameshinda tuzo ya mchezaji bora katika Ligi ya Mabingwa.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *