Riziki Pembe; Idara ya Elimu ya Watu wazima imepiga hatua katika kuanzisha programu, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on September 4, 2020 at 8:00 am

September 4, 2020

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar   Riziki Pembe  amesema Idara ya Elimu ya Watu wazima imepiga hatua katika kuanzisha programu zinazokwenda sambamba na mahitaji ya jamii zinazochangia katika kupambana na tatizo la ajira nchini.Akisoma hotu a kwa niaba yake wakati wa kilele cha maadhimisho ya Elimu ya watu wazima Duniani katika ukumbi wa Makonyo Wilaya ha chake chake Pemba, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo dkt Idrissa Muslim Hija amesema programu hizo zinaleta matumaini makubwa katika maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.Amesema elimu ya watu wazima imeanzishwa na waasisi wa nchi hii  Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambao waliipa kipaumbele Elimu hio baada ya kupata Uhuru wa nchi hizi kutokana  na kuelewa umuhimu wa Elimu ya watu wazima katika maendeleo ya haraka katika Taifa.Aidha mhe Riziki amewaomba wale wote ambao hawakufanikiwa kupata Elimu na umri wao nimeshakuwa mkubwa kuitumia fursa ya kujiunga na programu za Elimu ya watu wazima pamoja na vijana aaliokosa elimu ya Msingi nao wajisajili katika vya Elimu mbadala ili waweze kupata ujuzi utakaowasaidia kupambana na changamoto za maisha.Akizungumzia suala la utekelezaji wa majukumu ya Idara hiyo, mhe Riziki amesema hali hiyo inakwenda sambamba na sera ya Elimu ya mwaka 2006 ambayo inaeleza jukumu la uanzishwaji wa programu za Elimu ya watu wazima zitakazowanufaisha walengwa kupata waliokosa wakati wa mfumo rasmi wa Elimu pamoja na kuonesha hatua iliopatikana katika kuleta maendeleo endelevu kwa Taifa. Hata hivyo ameipongeza Idara hiyo kwa ujumla kwa hatua kubwa waliyofikia ambapo hali ya kisomo inaonekana kuimarika katika nchi na kuweza kutekeleza kwa vitendo ilani ya Chama Cha Mapinduzi. Nae Mkurugenzi Idara ya Elimu mbadala na watu wazima bi Mashavu Ahmada Fakih amesema lengo la kufanyika maadhimisho hayo ni kufanya tathmini ya hali ya kisomo katika nchi ambapo kwa Zanzibar hali  hiyo imeimarika kwa asilimia 84.2 juu ya wanaojua kusoma na kuandika.Amesema pamoja na kuwepo mafanikio hayo lakini bado kuna umuhimu kwa watu wa Elimu kuendelea kutoa ushirikiano katika kubuni mbinu mbalimbali za kuweza kuwasaidia wanakisomo kupata Elimu bora pamoja na kuwepo programu mbalimbali za TV na radio.Aidha ameishukuru viongozi mbalimbali wa mikoa katika kuwapa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha wanafanikiwa suala zima la tathmini ya watu wasiojua kusoma na kuandika ili waweze kuwasaidia. Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Taaluma Utafiti na ushauri wa Taasisi ya Elimu ya watu wazima Tanzania Bara bi Mary Watugulu amewashauri vijana kujiunga na vituo mbalimbali ili waweze kupata mikopo kwa urahisi itakayosaidia kuweza kujikwamua kutokana na suala zima la upatikanaji wa mitaji katika kazi zao.Akifunga kongamano hilo Katihu Mkuu  Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar dkt Idrissa Muslim  Hija amesema kongamano hilo limefanikiwa kwa asilimia kubwa kutokana na nzuri zilizowasilishwa pamoja na michango mizuri iliyotolewa na washiriki ambayo ina lengo la kuimarisha utoaji wa huduma bora za Elimu katika kituo hicho.Ameahidi kuwa michango yote iliyotolewa na wajumbe hao Wizara ya Elimu Zanzibar itayafanyia kazi na kuhakikisha maadhimisho ya mwakani yatakuwa yameshapatuwa ufumbuzi kwa asilimia kadhaa.Amesema tathmini ya watu wasiojua kusoma na kuandika inaendelea kufanywa ambapo kila Mkoa tayari zimeshaanza kufanyiwa kazi ili lengo la wananchi kujua kusoma na kuandika pamoja na kujitegemea liweze kufikiwa.Katika kongamano hilo pia aliwaasa wananchi kutokana na kuelekea uchaguzi Mkuu, kuwa makini katika kuendelea kuilinda amani ya nchi ili kwani bila ya amani hawataweza kupata Elimu hiyo na maendeleo yoyoten hayataweza  kupatikana katika nchi.Maadhimisho ya wiki ya Elimu ya watu wazima huadhimishwa kila ifikapo September 3 ya kila mwaka.,

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar   Riziki Pembe  amesema Idara ya Elimu ya Watu wazima imepiga hatua katika kuanzisha programu zinazokwenda sambamba na mahitaji ya jamii zinazochangia katika kupambana na tatizo la ajira nchini.

Akisoma hotu a kwa niaba yake wakati wa kilele cha maadhimisho ya Elimu ya watu wazima Duniani katika ukumbi wa Makonyo Wilaya ha chake chake Pemba, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo dkt Idrissa Muslim Hija amesema programu hizo zinaleta matumaini makubwa katika maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Amesema elimu ya watu wazima imeanzishwa na waasisi wa nchi hii  Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambao waliipa kipaumbele Elimu hio baada ya kupata Uhuru wa nchi hizi kutokana  na kuelewa umuhimu wa Elimu ya watu wazima katika maendeleo ya haraka katika Taifa.

Aidha mhe Riziki amewaomba wale wote ambao hawakufanikiwa kupata Elimu na umri wao nimeshakuwa mkubwa kuitumia fursa ya kujiunga na programu za Elimu ya watu wazima pamoja na vijana aaliokosa elimu ya Msingi nao wajisajili katika vya Elimu mbadala ili waweze kupata ujuzi utakaowasaidia kupambana na changamoto za maisha.

Akizungumzia suala la utekelezaji wa majukumu ya Idara hiyo, mhe Riziki amesema hali hiyo inakwenda sambamba na sera ya Elimu ya mwaka 2006 ambayo inaeleza jukumu la uanzishwaji wa programu za Elimu ya watu wazima zitakazowanufaisha walengwa kupata waliokosa wakati wa mfumo rasmi wa Elimu pamoja na kuonesha hatua iliopatikana katika kuleta maendeleo endelevu kwa Taifa. 

Hata hivyo ameipongeza Idara hiyo kwa ujumla kwa hatua kubwa waliyofikia ambapo hali ya kisomo inaonekana kuimarika katika nchi na kuweza kutekeleza kwa vitendo ilani ya Chama Cha Mapinduzi. 

Nae Mkurugenzi Idara ya Elimu mbadala na watu wazima bi Mashavu Ahmada Fakih amesema lengo la kufanyika maadhimisho hayo ni kufanya tathmini ya hali ya kisomo katika nchi ambapo kwa Zanzibar hali  hiyo imeimarika kwa asilimia 84.2 juu ya wanaojua kusoma na kuandika.

Amesema pamoja na kuwepo mafanikio hayo lakini bado kuna umuhimu kwa watu wa Elimu kuendelea kutoa ushirikiano katika kubuni mbinu mbalimbali za kuweza kuwasaidia wanakisomo kupata Elimu bora pamoja na kuwepo programu mbalimbali za TV na radio.

Aidha ameishukuru viongozi mbalimbali wa mikoa katika kuwapa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha wanafanikiwa suala zima la tathmini ya watu wasiojua kusoma na kuandika ili waweze kuwasaidia. 

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Taaluma Utafiti na ushauri wa Taasisi ya Elimu ya watu wazima Tanzania Bara bi Mary Watugulu amewashauri vijana kujiunga na vituo mbalimbali ili waweze kupata mikopo kwa urahisi itakayosaidia kuweza kujikwamua kutokana na suala zima la upatikanaji wa mitaji katika kazi zao.

Akifunga kongamano hilo Katihu Mkuu  Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar dkt Idrissa Muslim  Hija amesema kongamano hilo limefanikiwa kwa asilimia kubwa kutokana na nzuri zilizowasilishwa pamoja na michango mizuri iliyotolewa na washiriki ambayo ina lengo la kuimarisha utoaji wa huduma bora za Elimu katika kituo hicho.

Ameahidi kuwa michango yote iliyotolewa na wajumbe hao Wizara ya Elimu Zanzibar itayafanyia kazi na kuhakikisha maadhimisho ya mwakani yatakuwa yameshapatuwa ufumbuzi kwa asilimia kadhaa.

Amesema tathmini ya watu wasiojua kusoma na kuandika inaendelea kufanywa ambapo kila Mkoa tayari zimeshaanza kufanyiwa kazi ili lengo la wananchi kujua kusoma na kuandika pamoja na kujitegemea liweze kufikiwa.

Katika kongamano hilo pia aliwaasa wananchi kutokana na kuelekea uchaguzi Mkuu, kuwa makini katika kuendelea kuilinda amani ya nchi ili kwani bila ya amani hawataweza kupata Elimu hiyo na maendeleo yoyoten hayataweza  kupatikana katika nchi.

Maadhimisho ya wiki ya Elimu ya watu wazima huadhimishwa kila ifikapo September 3 ya kila mwaka.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *