Ridhiwani amuhakikishia Kinana ushindi mnono, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on September 1, 2020 at 1:00 pm

September 1, 2020

Na Omar Mngindo, MioniMGIMBEA Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Ridhiwani Kikwete, amemhakikishia Abdurhaman Kinana ushindi wa mnono kwa mgombea Urais Dkt. John Magufuli.Ridhiwani alitoa kauli hiyo katika viwanja vya shule ya Sekondari Kikaro, iliyoko Kijiji cha Miono Kata ya Miono jimboni humo, kwenye uzinduzi wa Kampeni ambapo Kinana alikuwa mgeni rasmi, aliyewatambulisha Ridhiwani, Muharami Mkenge na Madiwani 26.Alisema kuwa serikali ya Rais Magufuli ndani ya Jimbo la Chalinze na wilaya kwa ujumla imefanya mambo mengi makubwa, yanayokihakikishia ushindi mnono katika ychaguzu Mkuu utaofanyika Oktoba 28 mwaka huu.”Kiongozi wangu kwaniaba ya wana-Chalinze tunakihakikishia ushindi mkubwa chama chetu, hususani kwa mgombea wetu wa urais Dkt. John Magufuli, kwani tuna mengi ya kuyanadi kwenye kampeni yetu, ambayo yamefanywa na serikali yetu,” alisema Ridhiwani.Kwa upande wake Muharami Mkenge mgombea ubunge Jimbo la Bagamoyo alianza kuwashukuru wana-CCM la Bagamoyo kwa ushirikiano mkubwa katika kipindi chote, mpaka wakati huu wa kura za maoni na kuelekea kwenye uchaguzi Mkuu Oktoba 28.”Wana-Bagamoyo tunawahakikishia ushindi mnono kwenye uchaguzi wa Oktoba 28, wananchi wanaimani kubwa na Serikali yao inayoongozwa na chama chetu, chini ya Mwenyekiti wetu Dkt. John Magufuli kwani kubwa imefanyika na inaendelea kufanyika, tupelekee salamu zetu kwa mgombea wetu,” alisema Mkenge.Nae mgombea ubunge viti Maalumu Subira Mgalu alisema kuwa serikali yetu imetekeleza miradi mingi ikiweml ya kimkakati, akiitaja ya maji inayolenga kumtua mwanamke ndoo kichwani, akitaja uliopo Bagamoyo tenki lenye ujazo wa lita milioni 6, na wa mto Ruvu unaoelekea Chalinze.Akizungumza na mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo, Kinana alisema serikali inayoongozwa na na Rais Magufuli imefanya mambo mengi makubwa, hivyo amewaomba Wana-Bagamoyo wawachague wagombea wanaotokana na chama hicho ili wamalizie waliyoyaanza.”Sote ni mashahidi, kazi kubwa inafanywa na chama chetu chini ya Mwenyekiti Dkt. John Magufuli ambae ndio Rais anayeiongoza serikali mambo mengi makubwa ameyasimamia na sote tunayashuhudia,” alisema Kinana.Awali akizungumza na mamia hao, Mwenyekiti wa CCM wilaya Abdul Sharifu alisema kwamba chama hicho kina mtaji mkubwa wa wanachama, sanji na mambo ambayo yameshafanyika, hivyo amemtaka mgombea urais asiwe na hofu.,

Na Omar Mngindo, Mioni

MGIMBEA Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Ridhiwani Kikwete, amemhakikishia Abdurhaman Kinana ushindi wa mnono kwa mgombea Urais Dkt. John Magufuli.

Ridhiwani alitoa kauli hiyo katika viwanja vya shule ya Sekondari Kikaro, iliyoko Kijiji cha Miono Kata ya Miono jimboni humo, kwenye uzinduzi wa Kampeni ambapo Kinana alikuwa mgeni rasmi, aliyewatambulisha Ridhiwani, Muharami Mkenge na Madiwani 26.

Alisema kuwa serikali ya Rais Magufuli ndani ya Jimbo la Chalinze na wilaya kwa ujumla imefanya mambo mengi makubwa, yanayokihakikishia ushindi mnono katika ychaguzu Mkuu utaofanyika Oktoba 28 mwaka huu.

“Kiongozi wangu kwaniaba ya wana-Chalinze tunakihakikishia ushindi mkubwa chama chetu, hususani kwa mgombea wetu wa urais Dkt. John Magufuli, kwani tuna mengi ya kuyanadi kwenye kampeni yetu, ambayo yamefanywa na serikali yetu,” alisema Ridhiwani.

Kwa upande wake Muharami Mkenge mgombea ubunge Jimbo la Bagamoyo alianza kuwashukuru wana-CCM la Bagamoyo kwa ushirikiano mkubwa katika kipindi chote, mpaka wakati huu wa kura za maoni na kuelekea kwenye uchaguzi Mkuu Oktoba 28.

“Wana-Bagamoyo tunawahakikishia ushindi mnono kwenye uchaguzi wa Oktoba 28, wananchi wanaimani kubwa na Serikali yao inayoongozwa na chama chetu, chini ya Mwenyekiti wetu Dkt. John Magufuli kwani kubwa imefanyika na inaendelea kufanyika, tupelekee salamu zetu kwa mgombea wetu,” alisema Mkenge.

Nae mgombea ubunge viti Maalumu Subira Mgalu alisema kuwa serikali yetu imetekeleza miradi mingi ikiweml ya kimkakati, akiitaja ya maji inayolenga kumtua mwanamke ndoo kichwani, akitaja uliopo Bagamoyo tenki lenye ujazo wa lita milioni 6, na wa mto Ruvu unaoelekea Chalinze.

Akizungumza na mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo, Kinana alisema serikali inayoongozwa na na Rais Magufuli imefanya mambo mengi makubwa, hivyo amewaomba Wana-Bagamoyo wawachague wagombea wanaotokana na chama hicho ili wamalizie waliyoyaanza.

“Sote ni mashahidi, kazi kubwa inafanywa na chama chetu chini ya Mwenyekiti Dkt. John Magufuli ambae ndio Rais anayeiongoza serikali mambo mengi makubwa ameyasimamia na sote tunayashuhudia,” alisema Kinana.

Awali akizungumza na mamia hao, Mwenyekiti wa CCM wilaya Abdul Sharifu alisema kwamba chama hicho kina mtaji mkubwa wa wanachama, sanji na mambo ambayo yameshafanyika, hivyo amemtaka mgombea urais asiwe na hofu.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *