RC Zambi awataka wadau kutimiza wajibu wao kipindi cha ununuzi wa korosho, on September 17, 2020 at 10:00 am

September 17, 2020

Na Ahmad Mmow, Lindi.Wadau wa zao la korosho mkoani Lindi wametakiwa kutimiza wajibu wao kipindi cha ununuzi wa korosho ili kufanikisha ununuzi wa zao hilo msimu wa 20202021 ili kuepuka malalamiko na misuguano isiyo ya lazima.Zambi ametoa agizo hilo leo wakati wa kikao cha wadau wa korosho, ufuta na mbaazi katika mkoa wa Lindi ambacho kilifanyika  katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, manispaa ya Lindi.Alisema anakila sababu ya kuhimiza kila mdau atimize wajibu wake, kwani uzoefu unaonesha yanayokubaliwa kwenye vikao hayafanyiwi kazi kama ilivyokubaliwa. Badala yake kunakuwa na vitendo tofauti ambavyo vinasababisha usumbufu kwa wakulima.Akigusia eneo la ununuzi, Zambi aliwataka wanunuzi kulipa fedha za wakulima kwawakati kwamujibu wa makubaliano ili wakulima walipwe kwa wakati. Huku akiweka wazi kwamba kutolipa fedha za wakulima nikukiuka makubaliano. Kwahiyo kwa nafasi ya utawala na mamlaka aliyonayo hatasita kuwachukulia hatua wanunuzi watakao kiuka makubaliano.” Sitaona aya wala aibu, nitamchukulia hatua mtu yeyote atakayekiuka makubaliano. Madhali nalinda maslahi ya wakulima, ukigusa huko sikubali.Nawakuu wa wilaya msikubali,” alisisitiza Zambi.Aidha Zambi amewaonya wasafirishaji waache usumbufu na kukiuka makubaliano. Nikutokanana tabia ya kubadilisha bei za kusafirisha mazao kinyume na makubaliano.Kitendo ambacho kinasababishia gharama kubwa wakulima. Hivyo amewataka wakuu wa wilaya, hasa mkuu wa wilaya ya Kilwa kuhakikisha hali hiyo haitokei tena katika wilaya zao. Kwani katika wilaya ya  Kilwa wanunuzi walikiuka makubaliano na kuongeza bei mara nyingi.Zambi aliwanyooshea kidole viongozi na watendaji wa vyama vya msingi vya ushirika(AMCOS) kwabaadhi yao kutokuwa waaminifu japokuwa msimu wa 20192020 haujatokea wizi mkubwa. Hata hivyo kumekuwa na wizi mkubwa wa makusudi kwa wakulima wa ufuta wa wilaya za Liwale na Kilwa katika msimu wa 2020. Chama cha msingi cha ushirika Mirindimo kilichopo katika wilaya ya Liwale kikitajwa kuwa nikinara wa upotevu wa fedha za wakulima wa ufuta kwa msimu huo wa 2020.” Wapo maofisa ushirika wanashirikiana na viongozi wa AMCOS kuwaibia wakulima. Lakini pia wapo wanunuzi na maofisa ushirika wanaoshirikiana pia na viongozi wa AMCOS  kuwadhulumu wakulima,” alisisitiza Zambi.Mbali na hayo, Zambi amewataka mkuu wa wilaya ya Kilwa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo  wadhibiti njia zote zinazoingia wilayani humo ili korosho chafu zilizopo katika Mkoa wa Pwani ambazo msimu uliopita hazikuzwa ili zisiingie mkoani Lindi. Nikutokanana yeye kusikia ziko njama za kuingiza korosho hizo mkoani Lindi kwanjia zisizo halali.Amemtaka pia kamanda wa polisi wa Mkoa(RPC) wa Lindi kutoa ushirikiano wa kutosha kudhibiti korosho hizo zisiingie mkoani humu. Lakini pia aliwataka watumishi waliopo kwenye mizani za kupima uzito wa magari kuwa makini na kuzikagua gari za mizigo zinazotoka barabara ya  Dar-es-Salaam- Lindi- Mtwara ili kuhakikisha kama hazijapakiwa korosho hizo.,

Na Ahmad Mmow, Lindi.

Wadau wa zao la korosho mkoani Lindi wametakiwa kutimiza wajibu wao kipindi cha ununuzi wa korosho ili kufanikisha ununuzi wa zao hilo msimu wa 20202021 ili kuepuka malalamiko na misuguano isiyo ya lazima.

Zambi ametoa agizo hilo leo wakati wa kikao cha wadau wa korosho, ufuta na mbaazi katika mkoa wa Lindi ambacho kilifanyika  katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, manispaa ya Lindi.

Alisema anakila sababu ya kuhimiza kila mdau atimize wajibu wake, kwani uzoefu unaonesha yanayokubaliwa kwenye vikao hayafanyiwi kazi kama ilivyokubaliwa. Badala yake kunakuwa na vitendo tofauti ambavyo vinasababisha usumbufu kwa wakulima.

Akigusia eneo la ununuzi, Zambi aliwataka wanunuzi kulipa fedha za wakulima kwawakati kwamujibu wa makubaliano ili wakulima walipwe kwa wakati. Huku akiweka wazi kwamba kutolipa fedha za wakulima nikukiuka makubaliano. Kwahiyo kwa nafasi ya utawala na mamlaka aliyonayo hatasita kuwachukulia hatua wanunuzi watakao kiuka makubaliano.

” Sitaona aya wala aibu, nitamchukulia hatua mtu yeyote atakayekiuka makubaliano. Madhali nalinda maslahi ya wakulima, ukigusa huko sikubali.Nawakuu wa wilaya msikubali,” alisisitiza Zambi.

Aidha Zambi amewaonya wasafirishaji waache usumbufu na kukiuka makubaliano. Nikutokanana tabia ya kubadilisha bei za kusafirisha mazao kinyume na makubaliano.Kitendo ambacho kinasababishia gharama kubwa wakulima. Hivyo amewataka wakuu wa wilaya, hasa mkuu wa wilaya ya Kilwa kuhakikisha hali hiyo haitokei tena katika wilaya zao. Kwani katika wilaya ya  Kilwa wanunuzi walikiuka makubaliano na kuongeza bei mara nyingi.

Zambi aliwanyooshea kidole viongozi na watendaji wa vyama vya msingi vya ushirika(AMCOS) kwabaadhi yao kutokuwa waaminifu japokuwa msimu wa 20192020 haujatokea wizi mkubwa. Hata hivyo kumekuwa na wizi mkubwa wa makusudi kwa wakulima wa ufuta wa wilaya za Liwale na Kilwa katika msimu wa 2020. Chama cha msingi cha ushirika Mirindimo kilichopo katika wilaya ya Liwale kikitajwa kuwa nikinara wa upotevu wa fedha za wakulima wa ufuta kwa msimu huo wa 2020.

” Wapo maofisa ushirika wanashirikiana na viongozi wa AMCOS kuwaibia wakulima. Lakini pia wapo wanunuzi na maofisa ushirika wanaoshirikiana pia na viongozi wa AMCOS  kuwadhulumu wakulima,” alisisitiza Zambi.

Mbali na hayo, Zambi amewataka mkuu wa wilaya ya Kilwa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo  wadhibiti njia zote zinazoingia wilayani humo ili korosho chafu zilizopo katika Mkoa wa Pwani ambazo msimu uliopita hazikuzwa ili zisiingie mkoani Lindi. Nikutokanana yeye kusikia ziko njama za kuingiza korosho hizo mkoani Lindi kwanjia zisizo halali.

Amemtaka pia kamanda wa polisi wa Mkoa(RPC) wa Lindi kutoa ushirikiano wa kutosha kudhibiti korosho hizo zisiingie mkoani humu. Lakini pia aliwataka watumishi waliopo kwenye mizani za kupima uzito wa magari kuwa makini na kuzikagua gari za mizigo zinazotoka barabara ya  Dar-es-Salaam- Lindi- Mtwara ili kuhakikisha kama hazijapakiwa korosho hizo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *