RC Mtwara: Mnao Safiri, Safarini kwa Vibali Halali, on September 9, 2020 at 1:00 pm

September 9, 2020

Na Faruku Ngonyani,MtwaraRaia wa Taifa la Tanzania wametakiwa kutothubutu kusafiri kuelekea nchi jirani ya msumbiji bila kuwa na vibali au nyaraka halali zitazowatambulisha utaifa wao na kutumia vivuko rasmi vinavyotambulika ili kuepuka madhara ya kiusalama yanayoweza kujitokeza kutokana na ukiukwaji wa utaratibu na kiwezekana wasubiri hadi pale hali ya taifa hilo itakapo imarika.Kauli hii imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya uwepo wa taarifa zinazodai kuwa kuna raia wa nchi ya Msumbiji ambao wanakimbilia katika maeneo ya jirani na mpaka wa Tanzania na wengine kushambuliwa.Byakanwa amesema kuwa suala la kuwataka kutumia utaratibu huo unalenga kuimarisha ulinzi wa mipaka na kuendelea kujiridhisha juu ya kumbukumbu sahihi ya watanzania waliotoka na kuingia nchini.Amesema kuwa kutokana na kukauka kwa maji katika mto Ruvuma mpaka wa Tanzania na msumbiji unapitika kwa urahisi hata kwa kutembea na miguu.Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amekanusha uwepo wa taarifa kuwa machafuko yanayoendelea Msumbiji kuathiri taifa la Tanzania na kueleza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama nchini hapa vimejipanga imara kulinda usalama wa mipaka yake.,

Na Faruku Ngonyani,Mtwara

Raia wa Taifa la Tanzania wametakiwa kutothubutu kusafiri kuelekea nchi jirani ya msumbiji bila kuwa na vibali au nyaraka halali zitazowatambulisha utaifa wao na kutumia vivuko rasmi vinavyotambulika ili kuepuka madhara ya kiusalama yanayoweza kujitokeza kutokana na ukiukwaji wa utaratibu na kiwezekana wasubiri hadi pale hali ya taifa hilo itakapo imarika.

Kauli hii imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya uwepo wa taarifa zinazodai kuwa kuna raia wa nchi ya Msumbiji ambao wanakimbilia katika maeneo ya jirani na mpaka wa Tanzania na wengine kushambuliwa.

Byakanwa amesema kuwa suala la kuwataka kutumia utaratibu huo unalenga kuimarisha ulinzi wa mipaka na kuendelea kujiridhisha juu ya kumbukumbu sahihi ya watanzania waliotoka na kuingia nchini.

Amesema kuwa kutokana na kukauka kwa maji katika mto Ruvuma mpaka wa Tanzania na msumbiji unapitika kwa urahisi hata kwa kutembea na miguu.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amekanusha uwepo wa taarifa kuwa machafuko yanayoendelea Msumbiji kuathiri taifa la Tanzania na kueleza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama nchini hapa vimejipanga imara kulinda usalama wa mipaka yake.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *