RC Mtwara amaliza mgogoro wa wanandoa uliodumu miaka sita, on September 17, 2020 at 5:00 pm

September 17, 2020

 Na Faruku Ngonyani, Mtwara.Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa ametatua mgogoro wa ardhi kwa wanandoa baina ya Aziza Nyundo na aliyekuwa mume wake Salum Issa Namdidi ambao wamekuwa wakidaina eneo hilo kwa takriban miaka sita.Hatua hiyo imetokana na maamuzi ya mahakama ambapo iliwataka wanandoa hao kuchukua hatua ya kugawana mali au kuuza kisha kugawana fedha.Hata hivyo baada ya maamuzi hayo ya mahakama kukaibuka kikundi cha watu wa taasisi ya Dini ambao wameingilia kati mgogoro huo na kudai kuwa nyumba na eneo la ardhi ya wanandoa hao ni mali yao.Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amemuagiza kamanda wa polisi wilaya ya Mtwara kuwahoji watu hao kutokana na kuwa na nyaraka zinazoleta utata kwenye maelezo yaliyotolewa juu ya eneo hilo.Wakati hayo yakiendelea Mkuu wa Mkoa amemruhusu Aziza Nyundo kuendelea kubaki katika eneo hilo kwa kuwa nyaraka zake zilitolewa na mahakama zinaonyesha kwa sasa yeye ndiye mmiliki halali wa nyumba na ardhi katika eneo hilo.,

 Na Faruku Ngonyani, Mtwara.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa ametatua mgogoro wa ardhi kwa wanandoa baina ya Aziza Nyundo na aliyekuwa mume wake Salum Issa Namdidi ambao wamekuwa wakidaina eneo hilo kwa takriban miaka sita.

Hatua hiyo imetokana na maamuzi ya mahakama ambapo iliwataka wanandoa hao kuchukua hatua ya kugawana mali au kuuza kisha kugawana fedha.

Hata hivyo baada ya maamuzi hayo ya mahakama kukaibuka kikundi cha watu wa taasisi ya Dini ambao wameingilia kati mgogoro huo na kudai kuwa nyumba na eneo la ardhi ya wanandoa hao ni mali yao.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amemuagiza kamanda wa polisi wilaya ya Mtwara kuwahoji watu hao kutokana na kuwa na nyaraka zinazoleta utata kwenye maelezo yaliyotolewa juu ya eneo hilo.

Wakati hayo yakiendelea Mkuu wa Mkoa amemruhusu Aziza Nyundo kuendelea kubaki katika eneo hilo kwa kuwa nyaraka zake zilitolewa na mahakama zinaonyesha kwa sasa yeye ndiye mmiliki halali wa nyumba na ardhi katika eneo hilo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *