RC Mahenge akagua ujenzi wa kituo cha Afya Mtera, on September 8, 2020 at 8:00 am

September 8, 2020

Na Ezekiel Mtonyole, Mpwapwa.Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith mahenge ameridhishwa na kasi ya upanuzi wa ujenzi  wa kituo cha Afya Mtera kinachojengwa kwa shilingi milioni mia nne (400) ambacho kukamilika kwake  kutasaidia wananchi wa maeneo hayo na wasafari wanaotumia barabara Iringa Dodoma kupata huduma za Afya. Akitoa taarifa ya Kituo cha Afya cha Mtera, Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho, Getrudi Mosha amesema Kituo cha Mtera kimejengwa kwa msaada wa serikali ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli ambaye Aprili mwaka jana alipota hapo na akaona majengo ya kambi wakandarasi waliokuwa wakijenga barabara na kubadili matumizi na kukifanya kituo cha afya.Getrudi amesema baada ya agizo hilo, ili majengo hayo kukidhi mahitaji, serikali ilitoa sh milioni 400 ili kuongeza miundombinu mingine ili kituo hicho kiweze kutoa huduma bora kwa wenyeji na hata wasafiri wanaotumia njia hiyo.Katika kuoneshwa kuguswa na mchango wa serikali, wananchi wa eneo hilo walichangia sh milioni 3.6 ambazo zinatokana na kusafisha eneo, kukusanya mawe na mchanga ili kuwezesha ujenzi wa majengo matano.Hadi kufikia Agosti 30, mwaka huu fedha zilizotumika ni milioni 336.21 kati ya fedha hizo sh milioni 37.82 ni malipo ya mafundi, sh milioni 298.3 kwa ajili ya manunuzi ya vifaa na sh milioni 3.6 ambazo ni mchango wa jamii.Getrudi amesema ujenzi wa kituo hicho umefanyika kwa kutumia Force Akaunti kwa kusimamiwa na kamati tatu ambazo ni ya ujenzi, manunuzi na mapokezi na unatarajiwa kukamilika Septemba 30, mwaka huu.“Pamoja na changamoto kubwa mbili ikiwemo ya kutopatikana kwa maji kwa ajili ya ujenzi pamoja na uwepo wa mwamba mgumu, bado mradi huo unatazamiwa kukamilika ndani ya muda wake Septemba 30, mwaka huu,” amesema.Akisoma taarifa ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kinajengwa kwa ajili ya watu ambao walihamishwa kutoka mabondeni kutokana na mafuriko mwaka jana, Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho, Dominick Laurian alisema ujenzi huo ambao umekamilika kwa asilimia 95 unatazamiwa kukamilika Septemba 15, mwaka huu.Kituo hicho ambacho hadi Agosti 30, mwaka huu kimegharimu sh milioni 142.8 pamoja na sh milioni 2.5 za mchango wa kijamii na kufanya jumla y ash milioni 145.3, kimejengwa kwa mfumo wa force akaunti na kusimamiwa na kamati za ujenzi, manunuzi na mapokezi.Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Mahenge, kwanza amewapongeza viongozi wa Wilaya pamoja na kamati zilizosimamia kituo hicho kwa kazi nzuri na kwamba wananchi watapata huduma iliyobora bora.Pia Dkt Mahenge ameziagiza taasisi nyingine zinazohusika na ufikishaji wa miondombinu mingine kama maji na umeme kuhakikisha wanakaa pamoja na kuhakikisha huduma hizo zinafika katika kituo hicho  hakijaanza kutoka huduma kikamilifu zikiwemo za operesheni na uzalishaji.Dkt Mahenge amempongeza Rais Magufuli kwa kusema na kutekeleza kwa vitendo kauli yake ya kubadilisha majengo ya makandarasi na kukifanya kituo cha afya na kutoa fedha ili kuongeza miundombinu.Amesema Rais Magufuli ametoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa vituo na hospitali jumla 32 katika mkoa wa Dodoma vikiwemo vituo vya afya 26 ambavyo vimegharimu takribani sh bilioni 13 na hospitali sita ambazo zimegharibu takribani sh bilioni tisa.Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri amesema tayari kituo hicho kimeanza kufanya kazi tangu mwakajana na kukamilika kwa majengo hayo mapya kutasaidia kupanua huduma zilizokuwa hazipatikani katika maeneo hayo.Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa Dkt Binilith Mahenge amekagua pia uchenzi wa kituo cha Afya Chipogoro uliogharimu milioni mia mbili (200), Ujenzi wa Daraja la Chipogoro, ujenzi wa bara bara ya Chipogoro hadi Kibakwe na ujenzi wa bwalo katika shule ya Sekondari Kibakwe.,

Na Ezekiel Mtonyole, Mpwapwa.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith mahenge ameridhishwa na kasi ya upanuzi wa ujenzi  wa kituo cha Afya Mtera kinachojengwa kwa shilingi milioni mia nne (400) ambacho kukamilika kwake  kutasaidia wananchi wa maeneo hayo na wasafari wanaotumia barabara Iringa Dodoma kupata huduma za Afya. 

Akitoa taarifa ya Kituo cha Afya cha Mtera, Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho, Getrudi Mosha amesema Kituo cha Mtera kimejengwa kwa msaada wa serikali ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli ambaye Aprili mwaka jana alipota hapo na akaona majengo ya kambi wakandarasi waliokuwa wakijenga barabara na kubadili matumizi na kukifanya kituo cha afya.

Getrudi amesema baada ya agizo hilo, ili majengo hayo kukidhi mahitaji, serikali ilitoa sh milioni 400 ili kuongeza miundombinu mingine ili kituo hicho kiweze kutoa huduma bora kwa wenyeji na hata wasafiri wanaotumia njia hiyo.

Katika kuoneshwa kuguswa na mchango wa serikali, wananchi wa eneo hilo walichangia sh milioni 3.6 ambazo zinatokana na kusafisha eneo, kukusanya mawe na mchanga ili kuwezesha ujenzi wa majengo matano.

Hadi kufikia Agosti 30, mwaka huu fedha zilizotumika ni milioni 336.21 kati ya fedha hizo sh milioni 37.82 ni malipo ya mafundi, sh milioni 298.3 kwa ajili ya manunuzi ya vifaa na sh milioni 3.6 ambazo ni mchango wa jamii.

Getrudi amesema ujenzi wa kituo hicho umefanyika kwa kutumia Force Akaunti kwa kusimamiwa na kamati tatu ambazo ni ya ujenzi, manunuzi na mapokezi na unatarajiwa kukamilika Septemba 30, mwaka huu.

“Pamoja na changamoto kubwa mbili ikiwemo ya kutopatikana kwa maji kwa ajili ya ujenzi pamoja na uwepo wa mwamba mgumu, bado mradi huo unatazamiwa kukamilika ndani ya muda wake Septemba 30, mwaka huu,” amesema.

Akisoma taarifa ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kinajengwa kwa ajili ya watu ambao walihamishwa kutoka mabondeni kutokana na mafuriko mwaka jana, Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho, Dominick Laurian alisema ujenzi huo ambao umekamilika kwa asilimia 95 unatazamiwa kukamilika Septemba 15, mwaka huu.

Kituo hicho ambacho hadi Agosti 30, mwaka huu kimegharimu sh milioni 142.8 pamoja na sh milioni 2.5 za mchango wa kijamii na kufanya jumla y ash milioni 145.3, kimejengwa kwa mfumo wa force akaunti na kusimamiwa na kamati za ujenzi, manunuzi na mapokezi.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Mahenge, kwanza amewapongeza viongozi wa Wilaya pamoja na kamati zilizosimamia kituo hicho kwa kazi nzuri na kwamba wananchi watapata huduma iliyobora bora.

Pia Dkt Mahenge ameziagiza taasisi nyingine zinazohusika na ufikishaji wa miondombinu mingine kama maji na umeme kuhakikisha wanakaa pamoja na kuhakikisha huduma hizo zinafika katika kituo hicho  hakijaanza kutoka huduma kikamilifu zikiwemo za operesheni na uzalishaji.

Dkt Mahenge amempongeza Rais Magufuli kwa kusema na kutekeleza kwa vitendo kauli yake ya kubadilisha majengo ya makandarasi na kukifanya kituo cha afya na kutoa fedha ili kuongeza miundombinu.

Amesema Rais Magufuli ametoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa vituo na hospitali jumla 32 katika mkoa wa Dodoma vikiwemo vituo vya afya 26 ambavyo vimegharimu takribani sh bilioni 13 na hospitali sita ambazo zimegharibu takribani sh bilioni tisa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri amesema tayari kituo hicho kimeanza kufanya kazi tangu mwakajana na kukamilika kwa majengo hayo mapya kutasaidia kupanua huduma zilizokuwa hazipatikani katika maeneo hayo.

Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa Dkt Binilith Mahenge amekagua pia uchenzi wa kituo cha Afya Chipogoro uliogharimu milioni mia mbili (200), Ujenzi wa Daraja la Chipogoro, ujenzi wa bara bara ya Chipogoro hadi Kibakwe na ujenzi wa bwalo katika shule ya Sekondari Kibakwe.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *