Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara leo,

October 15, 2020

 

LEO Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea ambapo kutakuwa na michezo miwili kwa timu nne kusaka pointi tatu viwanja viwili tofauti.

Ratiba ipo namna hii Oktoba 15:- 

Gwambina iliyo nafasi ya 14 kwenye msimamo na pointi nne mchezo wake uliopita ilishinda mabao 2-0 dhidi ya Ihefu v Mtibwa Sugar iliyo nafasi ya 12 na pointi tano, mchezo wake uliopita ilifungwa bao 1-0 dhidi ya Biashara United Uwanja wa Gwambina saa 10:00 jioni.

Azam iliyo nafasi ya kwanza na pointi 15 mchezo wake uliopita ilishinda abao 4-2 dhidi ya Kagera Sugar  v Mwadui iliyo nafasi ya 10 na pointi 6 kibindoni.Mchezo wake uliopita ilishinda bao 1-0 dhidi ya Namungo FC, mchezo wa leo utachezwa Uwanja wa Azam Complex saa 1:00 usiku

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *