RaisTrump anasema anaendelea vizuri

October 12, 2020

Zaidi ya wiki moja baada ya kuambukizwa virusi vya corona, rais wa Marekani, Donald Trump, Jumapili, amesema anajisikia yuko vizuri sana, na hatumii dawa yoyote.

Katika mahojiano kwa njia ya simu na televijeni ya Fox news, Trump, amesema, “nimevishinda virusi hivi vibaya vya China, ni kama nina kinga ya mwili labda kwa muda mrefu, muda mfupi, labda maisha yangu yote.”

Lakini katika mahojiano hayo, mwanahabari hakumuuliza iwapo vipimo vilionyesha kwamba hana tena virusi vya corona, ambavyo vimesha ua zaidi ya watu laki mbili, na kuambukiza zaidi ya millioni saba ncini Marekani.

Muda mfupi baada ya kufanya mahojiano na televijeni ya Fox, Trump aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, kwamba madaktari wake wamethibitisha kuwa amepona kabisa, na kuongeza kuwa hivi sasa hawezi kuambukizwa Corona, wala hawezi kuwaambukiza watu wengine.

Baadae kampuni ya Twitter imesema “ujumbe wa Trump unakiuka maadili ya mtandao wa Twitter kuhusu kusambaza habari za uongo, na kupotosha za janga la Covid-19.

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *