Rais wa Uturuki ampongeza Amiri Mkuu mpya wa Kuwait Sheikh Nawaf al-Ahmad,

October 1, 2020

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan, amewasiliana na Amiri Mkuu mpya wa Kuwait Sheikh Nawaf al-Ahmad al-Jaber al-Sabah kwa njia ya simu.

Katika mazungumzo yao, rais Erdoğan alibainisha kuguswa na kifo cha aliyekuwa Amiri al-Ahmad al-Jaber al-Sabah, na kutuma salamu za rambirambi kwa jumuiya ya Kuwait pamoja na familia nzima kwa ujumla.

Rais Erdoğan pia alimpongeza as-Sabah kwa kukabidhiwa wadhfa kuwa Amiri mkuu mpya wa Kuwait huku akielezea matumaini yake ya kuboresha mahusiano ya kihistoria na kitamaduni baina ya Uturuki na Kuwait.

Rais Erdoğan aliongezea kusema kuwa nchi hizi mbili zitaendelea kuweka ushirikiano ili kudumisha amani na utulivu katika kanda husika.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *