Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron awasili Iraq, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on September 2, 2020 at 1:00 pm

September 2, 2020

 Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa leo hii amewasili nchini Iraq kwa ziara rasmi ya kikazi. Taarifa hiyo ni kwa mujibu shirika la habari la serikali ya Iraq. Macron, ambae alikuwa nchini Lebaon katika kipindi cha siku mbili zilizopita, amesema ziara yake hiyo ina lengo la kuanzisha mkakati mpya kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa, lakini alikataa kutoa ufafanuzi zaidi kutokana na sababu za kiusalama, ingawa alisema Iraq imekuwa katika wakati mgumu sana. Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha Iraq al-Sumaria, rais huyo wa Ufaransa atatumia masaa kadhaa nchini Iraq, kukutana na maafisa wa serikali, lakini pia kituo hicho hakikutoa ufafanuzi zaidi kuhusu safari hiyo. Wakati kundi la Dola la Kiislamu likitajwa kuendelea kuwa na nguvu katika baadhi ya maeneo kadha ya Iraq, mwezi Julai, Waziri Mkuu wa sasa Mustafa al-Kadhimi alitangaza kufanyika uchaguzi mkuu wa mapema wa bunge ifikapo 2021.,

 

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa leo hii amewasili nchini Iraq kwa ziara rasmi ya kikazi. Taarifa hiyo ni kwa mujibu shirika la habari la serikali ya Iraq. 

Macron, ambae alikuwa nchini Lebaon katika kipindi cha siku mbili zilizopita, amesema ziara yake hiyo ina lengo la kuanzisha mkakati mpya kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa, lakini alikataa kutoa ufafanuzi zaidi kutokana na sababu za kiusalama, ingawa alisema Iraq imekuwa katika wakati mgumu sana.

 Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha Iraq al-Sumaria, rais huyo wa Ufaransa atatumia masaa kadhaa nchini Iraq, kukutana na maafisa wa serikali, lakini pia kituo hicho hakikutoa ufafanuzi zaidi kuhusu safari hiyo. 

Wakati kundi la Dola la Kiislamu likitajwa kuendelea kuwa na nguvu katika baadhi ya maeneo kadha ya Iraq, mwezi Julai, Waziri Mkuu wa sasa Mustafa al-Kadhimi alitangaza kufanyika uchaguzi mkuu wa mapema wa bunge ifikapo 2021.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *