Rais wa mpito Bolivia atoa wito wa uvumilivu baada ya kura,

October 19, 2020

Rais wa mpito wa Bolivia Jeanine Anez ametoa wito wa uvumilivu na kuwataka raia waepuke kufanya vurugu wakiwa wanasubiri kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa jana Jumapili. 

Matokeo yanatarajiwa kutolewa polepole kuliko kawaida baada ya Mahakama ya Uchaguzi kuzuia uhesabuji kura wa haraka uliozoeleka, kwa lengo la kupatikana matokeo yenye uhakika zaidi. 

Licha ya kampeni zilizokuwa na hamasa za kisiasa, uchaguzi ulifanyika kwa amani, baada ya kuahirishwa mara mbili tofauti kutokana na kitisho cha virusi vya corona. 

Aidha ni uchaguzi wa kwanza katika kipindi cha miaka 20 ambao haukumshirikisha rais wa zamani Evo Morales.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *